Mkutano wa mawaziri wa afya jumuiya ya nchi za sadc kufanyika novemba 04-08/2019 jijini dar es salaamWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya maandalizi
ya Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Afya na UKIMWI kutoka Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam
kuanzia tarehe 04 hadi 08 Novemba 2019,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati
akitoa taarifa ya maandalizi ya Mkutano huo kulia ni Dkt. Leonard Subi
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia,
Wazee, na Watoto.Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Zamaradi Kawawa akoa ufafanuzi masuala kadhaa katika mkutano huo.Baadhi ya wataalam kutoka wizara ya Afya na Tume ya Kudhibiti Ukimwi TACAIDS wakiwa katika mkutano huo.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati
akitoa taarifa ya maandalizi ya Mkutano huo kushoto ni Dkt. Zainad
Chaula Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.


…………………………………………………


Na John Bukuku


Tanzania inatarajiwa kuwa
mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Afya na UKIMWI kutoka Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa
kufanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar
es Salaam kuanzia tarehe 04 hadi 08 Novemba 2019.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu amesema hayo wakati akitoa taarifa ya maandalizi ya mkutano huo
kwenye ukumbi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) jijini Dar
es salaam leo.


Waziri Ummy Mwalimu amesema
Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Afya na UKIMWI unatarajiwa kufunguliwa
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan.


Amesema Mkutano wa Mawaziri wa
Sekta ya Afya na UKIMWI unalenga kuangalia hatua iliyofikiwa katika
utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC ya mwaka 1999 na Mpango Mkakati
wa Kanda kuhusu masuala ya Afya pamoja na kuridhia kwa pamoja maazimio
mbalimbali kuhusu masuala ya afya kwa nchi za SADC.


“Agenda zitakazojadiliwa katika
mkutano huo ni Magonjwa ya kuambukiza yanayoziathiri nchi za SADC kama
vile Kifua Kikuu, Malaria na UKIMWI, Masuala ya lishe na Uimarishaji wa
Mifumo ya Afya” Amesema Ummy Mwalimu.


Ameongeza kuwa Bado nchi zote
kumi na sita zina changamoto za maambukizi ya UKIMWI,Tanzania tumeweza
kupunguza maambukizi kutoka asilimia 7 mwaka 2003 hadi asilimia 4.7
mwaka 2017 na bado juhudi za kuchukua hatua ili kupunguza zaidi
maambikuzi ya UKIMWI zinaendelea.


Kwa upande wa ugonjwa wa kifua
kikuu Kidunia nchi thelathini zinazobeba mzigo mkubwa wa Kifua
Kikuu(TB),Tanzania ipo katika nchi tano kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) zinazokabiliwa na ugonjwa huu.


Tanzania imefanikiwa kuwa
miongoni mwa nchi 10 zilizofanikiwa katika kuwaibua wahisiwa wa ugonjwa
wa TB, ambapo Mgonjwa wa TB akitumia dawa vizuri anapona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *