Mkuu wa mkoa singida dkt. rehema nchimbi atekeleza agizo la waziri mkuu

 Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akizungumza na wananchi wenye
kero mbalimbali dhidi ya serikali mjini hapa jana, ambao walimuonesha
mabango ya kero hizo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa kwenye ziara
ya kikazi mkoani hapa mapema mwezi huu.
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani)
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani)
 Mkutano ukiendelea
 Mama akitoa kero yake kwa maofisa wa idara za serikali mkoani Singida katika mkutano huo.
Maofisa wa idara za serikali mkoani Singida, wakipokea kero za wananchi hao (hawa pichani
 
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
 
MKUU
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amekutana na wananchi wenye
kero mbalimbali dhidi ya serikali ambao walimuonesha mabango ya kero
hizo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani
hapa mapema mwezi huu.
 
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuyaona na kupokea mabango hayo
alimuagiza mkuu wa mkoa kutatua changamoto za wananchi hao ambapo jana
alikutana nao akiwa na viongozi wa idara za serikali kwa ajili ya
kuwasikiliza na kutafuta njia ya kuzitatua kwa pamoja.
 
Hata
hivyo ilitokea sintofahamu baina ya wananchi hao na mkuu wa mkoa huo
pale walipotakiwa kusikilizwa na viongozi wa idara za serikali ambao
walishindwa kuzitatua hapo awali na kufikia uamuzi wa kumuonesha mabango
waziri mkuu.
 
Pamoja
na sintofahamu hiyo baadae wananchi hao walikubali kusikilizwa  ambapo
mkuu huyo wa mkoa aliwagiza viongozi hao hasa wa Manispaa ya Singida
kupanga tarehe za kukutana na wananchi hao wengi wakiwa na malalamiko ya
migogoro ya ardhi.

 

Baadhi ya malalamiko waliyoyatoa kwa Waziri

Mkuu
Kassim Majaliwa ni pamoja na madai ya fidia ya viwanja namba 23 na eneo
lililoko nyuma ya moja ya kiwanja cha Ginnery, kupinga rufaa ya kesi ya
ardhi iliyotoleea hukumi na baraza la ardhi la wilaya ya Singida.
 
Madai
mengine ni kiwanda cha mafuta ya alizeti kumilikiwa na wajanja
wachache, kutokamilika kwa mradi wa ujenzi wa matundu ya vyoo na mabweni
shule ya msingi Mtinko tangu mwaka 2017 na mkopo wa Saccos fedha kutoka
NSSF 160 milion zilizokuwa wakopeshwe wanachama wamekopeshwa vigogo
kutoka Singida mjini.
 
Mkazi
wa Kata ya Mwankoko Rochard Katyani ambaye ana malalamiko ya fidia ya
ardhi aliomba serikali kumaliza malalamiko ya migogoro ya ardhi
ambayoimedumu kwa mda mrefu.
 
Kati
ya migogoro 27 iliyowasilishwa kwa waziri mkuu kwa njia ya mabango
migogoro zaidi ya 20 inahusu masuala ya ardhi hasa fidia baada ya ardhi
za wahusika kudaiwa kuchukuliwa na serikali kwa matumizi mengine.