Mkuu wa mkoa wa shinyanga azindua chanjo ya surua, rubella na polio




Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amezindua Kampeni ya kitaifa ya
Chanjo ya Surua, Rubella na Polio, mkoa wa Shinyanga ambayo itatolewa
kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ili kuwapatia kinga dhidi
ya magonjwa hayo.

Uzinduzi
wa chanjo hiyo umefanyika leo Oktoba 17, 2019 katika kata ya Lyabukande
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, na kuhudhuriwa na wananchi wa kata
hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo wataalamu wa
afya ngazi ya mkoa na wilaya.

Akizungumza
kwenye uzinduzi huo Telack amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania chini ya Rais Dkt. John Magufuli, inathamini afya za wananchi
wake hasa katika kuzuia magonjwa yanayozuilika kwa chanjo na ndiyo maana
chanjo hiyo inatolewa bure.

“Nawaombeni
wazazi wote mkoani Shinyanga mjitokeze kwa wingi kupeleka watoto wenu
wenye kuanzia umri wa miezi tisa hadi 49 yaani miaka Minne na miezi 11
kupatiwa chanjo hii ya Surua, Rubella na polio ili kuwapatia kingi dhidi
ya magonjwa haya”,amesema Telack.

“Ugonjwa
wa Surua una madhara makubwa kwa watoto ambapo unaweza kumsababishia
madhara ya upofu, kuhara, na utapiamlo, Rubela unaweza kumsabishia mtoto
ulemavu, magonjwa ya moyo na mtoto wa jicho, Polio unaweza kumsabishia
mtoto kupooza mwili wote, hivyo nawataka wazazi msipuuzie zoezi
hili,”ameongeza.

Pia
amewaonya wananchi ambao watapotosha zoezi hilo la utoaji chanjo kwani
baadhi yao wamekuwa na tabia ya kufanya upotoshaji, na kubainisha kuwa
atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Naye
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume, ametaja takwimu za
watoto ambao watapewa chanjo hiyo kwa mkoa mzima kuwa ugonjwa wa Surua
na Rubella watafikiwa watoto 286,124 na Polio watoto 151,547.

Amesema
zoezi hilo limeanza leo Oktoba 17 na litakoma tarehe 21 mwaka huu,
ambapo huduma hiyo itatolewa kwenye maeneo yote ya huduma za afya mkoa
wa Shinyanga.

Nao
baadhi ya wazazi ambao walifika kwenye uzinduzi huo wa chanjo, pamoja
na watoto wao kuanza kupatiwa chanjo hiyo akiwamo Monica Shija,
wameipongeza Serikali kwa kujali afya za watoto wao na kuwapatia kinga.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati akizindua
chanjo ya Surua, Rubella na Polio leo Alhamis Oktoba 17,2019 katika 
kata ya Lyabukande halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Chanjo hiyo itatolewa kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano. Picha zote na Marco Maduhu – Malunde 1 blog

Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, akionya wananchi kuacha
kupotosha juu ya utolewaji wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.


Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akitoa wito kwa wazazi
kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto wao waliochini ya umri wa miaka
mitano kupatiwa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.


Mganga
mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akizungumza kwenye
uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Surua, Rubella na Polio namna itakavyo
saidia kukinga watoto dhidi ya magonjwa hayo.


Mwananchi Monica Shija akiishukuru serikali kwa kutoa chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Kushoto
ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, akizindua chanjo ya
Surua, Rubella na Polio kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.


Dkt. Geofrey Anthony akitoa chanjo ya Surua, Rubela na Polio kwa mtoto.

Muuguzi
wa Zahanati ya Lyabukande Godfrey Mbelela (kulia), akitoa maelezo kwa
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe.Zainabu Telack namna watakavyotoa huduma
ya chanjo ya Surua, Rubella na Polio.


Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Wananchi wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Kikundi cha sanaa cha Shinyanga kikitoa Burudani kwenye uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubella na Polio.

Awali
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwasili kwenye uzinduzi
wa Kampeni ya Chanjo ya Surua, Rubella na Polio, kwenye Kata ya
Lyabukande halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.


Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akipiga picha ya pamoja na baadhi ya
wazazi waliopeleka watoto wao kupatiwa Chanjo ya Surua, Rubella na
Polio, wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta
Mboneko, na wakwanza mkono wa kushoto ni mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba.