Mkuu wa mkoa wa shinyanga mhe. mndeme atoa maagizo kwa maafisa tarafa, watendaji wa kata, mitaa na vijiji

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
amewaagiza maafisa Tarafa, Watendaji  wa kata, Mitaa na vijiji kusimamia
matumizi ya fedha za Miradi ya maendeleo 
ambazo zinatolewa na serikali katika maeneo yao.

Ametoa maagizo hayo leo wakati akizungumza na maafisa
tarafa, watendaji wa kata, Mitaa na vijiji kutoka katika Halmashauri za
Kishapu, Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

RC Mndeme amewataka viongozi hao kwenda kutekeleza
maelekezo ya Rais  Dkt.Samia Saluhu Hassan
kwa vitendo, katika sekta zote ambazo Serikali inatoa fedha kwa ajili ya
kugharamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya Afya, Elimu na
miundombinu.

“Nendeni
mkatafadhiri kwa vitendo maono ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amedhaminia kuwaletea maendeleo watanzania sisi
watendaji tunaowajibu wa kusimamia shughuli za maendeleo zote katika maeneo
yetu nendeni mkatafadhiri maono ya Mhe. Rais kwa vitendo katika sekta zote sekta
ya maji, sekta ya viwanda, sekta ya barabara, sekta ya afya , sekta ya elimu na
sekta zingine zote bila uoga kasimamieni maono ya Mhe. Rais kwa ujasili
ilimradi usivunje sheria”.

“Nendeni
mkasimamie utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yenu fedha
zinaziletwa na Mhe. Rais zisimamiwe kikamilifu pawepo na matumizi sahihi ya
miradi lakini pia miradi ikamilike kwa wakati na kwa ubora, kasimamieni
utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi wa vitendo”.amesema RC Mndeme

“Nendeni
mkasimamie na kupinga kwa vitendo ukatili dhidi ya watoto ikiwa ni pamoja na
kuchukua hatua stahiki kwa wale wote ambao wanafanya ukatili kwenye jamii iwe
ni ukatili wa watoto iweni ni ukatili wa wanawake na wanaume nendeni mkasimamie
na kupinga ukatili huo likiwemo suala la ndoa za utotoni sasa tukisikia ndoa ya
mwanafunzi imefungwa mtendaji wa eneo utajieleza ulikuwa wapi niwaombe sana
wakurugenzi lisimamieni hili kuweni karibu na jamii zuieni vitendo vya ubakaji
na ulawiti”.amesema RC Mndeme

“Simamieni
ukusanyaji wa mapato hakikisheni hakuna mianya yoyote ya kuvuja kwa mapato ya
Halmashauri na vilevile ongezeni vyanzo vya mapato katika maeneo yenu waambieni
wananchi fedha zilizopokelewa za miradi katika maeneo yetu suala lingine ni
ulinzi na usalama hakikisheni kila mmoja eneo lake linakuwa salama kuweni na
orodha ya wakazi katika maeneo yetu jiepushenui kupokea watu msiowafahamu
likiwemo suala la wahamiaji haramu mkalisimamie”.

“Ninyi
watendaji mnawajibu wa kutatua kero za wananchi katika maeneo yetu msisubiri
mpaka viongozi wa juu nitahitaji kupata taarifa za utatuzi wa kero za wananchi
za kila mwezi wasilisheni kwa makatibu tawala wa Wilaya, fungueni milango wazi
lakini pia punguzeni kuchati na simu au kuongea na simu wakati wa kumhudumia
wananchi nendeni mkawahudumie wananchi bila ubaguzi”.amesema RC Mndeme

“Nendeni
mkasimamie na kuzuia utoro shuleni wale watoto wote walioacha shule nendeni
mkawarudishe darasani ni haki yake motto kupata elimu, lakini pia nendeni
mkatatue migogoro ya ardhi na mhakikishe mnazuia migogoro ya ardhi kwenye
maeneo yenu pia mkazuie migogoro ya wakulima na wafugaji  tuishi kwa utii wa sheria”.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amezungumzia
uwepo wa mvua nyingi za wastani katika Mkoa wa Shinyanga huku akiwaagiza
watendaji hao kutoa taarifa za tahadhari ya mvua kwa wananchi.

“Nendeni
mkawaambie wananchi wachukue tahadhari ya mvua kwa kuwashirikisha maafisa ugani
walime mazao ambayo yatafaa kwenye mvua hizi nyingi nendeni mkawaambie wananchi
walioko kwenye maeneo hatarishi wachukue tahadhari na kuondoka kwenye maeneo hayolakini
pia kasimamieni utunzaji wa mazingira pamoja na kuzingatia suala la usafi wa kila
Jumamos ya mwisho wa mwezi”. Amesema RC Mndeme

 Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Johari
Samizi amewasisitiza viongozi hao kushirikiana na wananchi hasa katika hatua za
utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika maeneo yao.

Nao baadhi wa watendaji wa kata, mitaa na vijiji
wameahidi kutekeleza maagizo hayo kwa kufuata taratibu za Nchi.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga, leo ameshiriki katika
kikao cha pamoja na Maafisa tarafa, watendaji wa kata, Mitaa na vijiji kutoka
katika Halmashauri tatu za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga na Shinyanga
vijijini.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano
Savana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mkuu wa Wilaya
ya Shinyanga Johari Samizi, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na wajumbe wa
kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akitoa
maagizo kwa maafisa Tarafa, Watendaji  wa kata, Mitaa na vijiji kutoka
katika Halmashauri za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya
ya Shinyanga leo Jumanne Oktoba 10,2023.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akitoa
maagizo kwa maafisa Tarafa, Watendaji  wa kata, Mitaa na vijiji kutoka
katika Halmashauri za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya
ya Shinyanga leo Jumanne Oktoba 10,2023.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi akizungumza
kwenye kikao hicho leo Jumanne Oktoba 10,2023.

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa
Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike
akiomba ushirikiano kwenye
kikao hicho leo Jumanne Oktoba 10,2023.

Kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina
Mndeme na  maafisa Tarafa,
Watendaji  wa kata, Mitaa na vijiji kutoka katika Halmashauri za Kishapu,
Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kikiendelea leo
Jumanne Oktoba 10,2023 katika ukumbi wa Savana.