Mmewe shinyanga mwanamke auawa kwa kuvunjwa shingo na mmewe shinyanga

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Mwanamke aitwaye Pendo Nena (20) mkazi
wa kijiji cha Mwanima, kata ya Busangwa wilaya ya Kishapu na mkoa wa
Shinyanga ameuawa kwa kunyongwa na kuvunjwa shingo na mmewe John Paulo
(27) kutokana na wivu wa mapenzi. 

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa
Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Novemba 3,2019 majira
ya saa tatu asubuhi ambapo mwanamke huyo aliuawa kwa kunyongwa shingo
yake ndani ya chumba chao cha kulala. 

“Baada ya kufanya mauaji hayo John
Paulo alikwenda katika kijiji cha Mwakolomwa na kujinyonga juu ya mti
kwa kutumia kamba ya chandarua.

 Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi. Mbinu iliyotumika ni kumnyonga shingo na kuivunja”,amesema Kamanda Abwao. 

Kamanda Abwao anatoa wito kwa wananchi
kufuata Sheria za nchi, sambamba na kuomba ushirikiano wa viongozi wa
dini katika kuelimisha jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *