Mrema alalamika kuchezewa rafu uchaguzi serikali za mitaa

Mwenyekiti
wa chama cha TLP, Augustino Mrema, amesema anaenda kulalamika kwa Rais
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kile alichokidai mgombea wa
chama chake kufanyiwa hujuma, ili mgombea wa Chama Cha Mapinduzi ashinde
Uenyekiti wa Serikali za Mitaa katika Kijiji alichozaliwa yeye cha
Kiraracha.


Mrema
amedai katika zoezi hilo walijitokeza baadhi ya watu, yeye mwenyewe
hakuwafahamu walimlazimisha wakala wake kunywa bia, wakati zoezi la
kupiga kura likiwa linaendelea huku wakala wake akikataa kufanya hivyo.

“Wananchi
wangu walimuona Mwenyekiti wao wa zamani aliyekaa miaka 10 anafaa
kuendelea kuwaongoza, nilichoshangaa ni kuwa nguvu kubwa ilitumika, kwa
sababu kulikuwa na idadi kubwa ya Polisi na wengine walilazimika kuleta
bia ili wakala wangu anywe.” Amesema Mrema

“Walipoleta
bia, wakala wangu alikataa basi wakatumia hiyo nafasi kufanya mgombea
wa chama kingine ashinde nafasi hiyo, kilichonishangaza Vijiji vyote
havikukubaliwa wagombea wetu ni Kijiji kimoja tu.”

Jana
Novemba 24, 2019 Watanzania wa maeneo mbalimbali nchini, walishiriki
zoezi la kupiga kura kwa kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa,
Vijiji pamoja na Vitongoji.