Msaada wa vifaa vya corona kwa waandishi arusha waendelea kumtesa wakili msando polisi

Wakili Albert Msando kushoto akimkabidhi kitakasa mikono Mwenyekiti wa Klabu ya wandishi wa habari Arusha Claud Gwandu. Msando alitoa msaada huo kwa lengo la kuwanusuru waandishi wa habari wa Arusha na maradhi ya Corona
Na Mwandishi Wetu, Arusha

JESHI La polisi Arusha limeeleza sababu ya kumshikilia Wakili Maarufu nchini Albert Msando kwa kile wanachodai kuwa ni kueneza maneneo ya uchochezi kuhusu ugonjwa wa Corona.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Moita Koka Wakili Msando juzi, Jumanne Aprili 26 akiwa anagawa vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa waandishi wa habari Mkoa wa Arusha kupitia Klabu yao ya waandishi wa Habari, alisema hali ya ugonjwa wa Corona ni mbaya sana.

Koka amewaeleza waandishi wa habari kuwa kupitia video clip iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii Wakili Msando alieleza kuwa hali ya ugonjwa wa Corona ni mbaya sana na kwamba kufanya hivyo ni kinyume kwa kuwa hana mamlaka ya kufanya hivyo.

“Ukweli ni kwamba na niseme bila kufika hali ni mbaya kwa Arusha na ndugu waandishi nyinyi lazima mfike mahali muweke mfuu chini mseme ukweli ili wananchi na serikali na kila anayehusika atambue kwamba tupo katika hali mbaya, ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuhcukua hatua mkirudi nyuma na kuogopa kusema tutazikana,” alinukuu kauli ya Msando.

Kwa mujibu wa Koka, upelelezi dhidi ya Wakili Msando unaendelea na mahojiano yakimalizika atafikishwa mahakamani.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Arusha, Claud Gwandu alitakiwa kufika katika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha saa nane mchana Aprili 30, 2020 kwa mahojiano kuhusiana na hatua ya wakili Msando kutoa msaada kwa waandishi wa habari.

Hata hivyo kwa Mujibu wa Claud Gwandu alitii amri aliyoagizwa  lakini alipofika alielezwa kuondoka na kutakiwa kuendelea na shughuli zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *