Mshukiwa wa kwanza wa virusi vya corona aripotiwa nchi jirani ya kenya

Taarifa zinaeleza kuwa mtu mmoja anayeshukiwa kuwa na virusi vya Corona nchini Kenya amepelekwa hospitalini.


Mshukiwa
huyo amefikishwa hospitali kuu ya rufaa ya Kenyatta. Vyombo vya habari
nchini humo vimeripoti kuwa mtu huyo aliwekwa karantini alipowasili
katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Hapo Jana Kenya iliitahadharisha raia wake kwenda mji wa Wuhan China, mpaka pale mlipuko wa virusi hivyo utakapodhibitiwa.

Wizara
ya mambo ya nje ya nchi hiyo ilisema ilikuwa na mawasiliano na raia
wake waliokwama katika mji wa Wuhan, mji ambao ni kitovu cha mlipuko wa
virusi hivyo, ambao uko kwenye uangalizi maalum.

”Ubalozi
unafahamu kuwa kuna raia wa Kenya 85 mjini Wuhan ambao wamesajiliwa
ubalozini hivyo unafuatilia kwa karibu hali hiyo,” wizara ilieleza
kwenye taarifa yake hapo jana.

-BBC