Mtalii afariki akiruka angani na parachuti kutoka kilele cha mlima kilimanjaro

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Justin Kyllo (51), raia wa Canada amekufa baada ya Parachuti alilokuwa
akitumia kuruka angani kutoka kilele cha mlima Kilimanjaro nchini
Tanzania kugoma kufunguka.
Akizungumza leo Jumamosi Septemba 28, 2019 kamishna msaidizi mwandamizi
wa Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete amethibitisha kifo cha
mtalii huyo, kwamba kimetokea katika kituo cha Stella Point kilichopo
katika mlima huo.
Amesema mtalii huyo alifika Septemba 20, 2019 kwa ajili ya kupanda
mlima, leo asubuhi alitumia Parachuti kwa ajili ya kuruka angani ili
kushuka chini ya mlima lakini iligoma kufunguka na kusababisha kifo
chake.