Mufti zuberi awafunda watanzania, awataka kuziishi tabia za mtume


Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mufti wa Tanzania Sheikh,Abuubakari Zuberi amewataka waislamu
na watanzania  nchini kujenga ushirikiano
na kusaidiana kwa kuiga tabia za Mtume Muhammad S.W.A kwa kuziishi tabia zake na
kuendana na mambo yalio mema na mwisho kufanyakazi kulijenga taifa bila
kulalamika wala migogoro.
Mutfi Zuberi ameyasema jijini hapa akiwa katika ziara yake ya
siku mbili mkoani hapa baada ambapo aliwataka waislamu kuendelea kuidumisha
amani ya nchi kwa lengo la kuondoa migogoro baina yao.


Amesema kuishi kwa vifundo sio maagizo ya uislamu na kuwataka
wale wenye vifundo vyao waache na kurudi kwa Mwenyezi Mungu kwa kile alichodai
kuwa hakuna anayeijua kesho yake hivyo busara ni kuwa wachamungu kuishi kwa
kuvumiliana na subra ndio muongozo.
Amesema kuwa maisha ya waislamu yawe ni sehemu ya kiigizo
chema kwa wengine kwa kuiga tabia za mtume Muhammad s.w.a kama alivyofanya kwa
watu wa twaifu, kwa kutanguliza umma mbele badala ya kuwa sehemu ya kuangamiza.
“Busara kwenu sio migogoro ambayo imekuwa ikirudisha shughuli
za maendeleo nyuma wala tusiwe watu wa kulalamika kila mara tuchape kazi kwa
kujiletea maendeleo na kufanya ibadat hilo ndio lengo la uislamu na hiyo ndio jihad”amesema
Mufti Zuberi.
Kwa mujibu wa Mufti Zuberi niwaombe waislamu wote nchi nzima
tuishi kwa kupendana na kuheshimiana kwa minajili ya kutaka radhi za Allah na
kuwatendea wema wenzetu iwe ni kiigizo chema kuwavuta kwenye dini.
Aidha amewataka kuondokana na mitazamo yenye chuki baina yao
na kuijenga jamii yenye ustaarabu kwani uislamu unajengwa na mambo mawili
makubwa kujitoa na kujitolea katika dini na maisha yao hivyo waishi kwa kufuata
misingi ya dini kwa kuwa tuna kitabu kitukufu Quraan turudi huo pindi
tunapohitilafiana.
Akatanabaisha kuwa amani ndio nguzo ya kuabudu kwa misingi ya
kuijenga amani nchini kwani bila amani ibada yenye kutulia haipo kwa kuwa
uislamu ulifika hadi Hispania lakini walipopiasha waliharibu kila kitu hadi
bahari ikawa nyekundu kutokana na wino wa vitabu hivyo busara ndio iwe nguzo ya
kuondoa changamoto naina yao.