Mume atolewa utumbo nje na mkewe kisa kuhoji matumizi ya shilingi elfu 10 aliyoacha

Benedictor
Gogogo (48) mkazi wa Itabagumba, Sengerema mkoani MWANZA amechanwa
tumbo na kitu chenye ncha kali hadi utumbo kutoka nje baada ya kutokea
ugomvi kati yake na mke wake

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Jumanne Murilo amesema tukio hilo
lilitokea jana na wanamashikilia Mtuhumiwa kwa mahojiano na uchunguzi
zaidi
Akiwa hospitalini, Gogogo amesema mzozo kati yake na mke wake aliyemtaja
kwa jina la Mama Asteria ulitokana na kuhoji matumizi ya Tsh. 10,000
aliyoacha nyumbani asubuhi ya siku hiyo
Amesema, “Wakati naondoka kwenda kwenye shughuli zangu za uvuvi, asubuhi
ya siku ya tukio, niliacha Tsh. 10,000 ya matumizi. Niliporejea
nilimwomba anipe Tsh. 1,000 ninunulie vocha ya simu lakini akaniambia
fedha yote imeshatumika.”
Ameongeza, “Nilipohoji zaidi akaanza kunitolea majibu yaliyonikasirisha
na kunifanya nimpige kofi na kutokea mzozo kati yetu ambao hata hivyo
uliisha na mimi kuingia ndani kujipumzisha.”
Aidha, Gogogo ameeleza kuwa akiwa ameanza kupitiwa usingizi, mke wake
ambaye wameishi mwaka mmoja na nusu sasa alimvizia na kumchana na kitu
chenye ncha kali tumboni hadi utumbo kutoka nje