Muuguzi asakwa kwa kumbaka aliyekuwa akimuuguza mama yake, ‘alimdunga sindano ya usingizi mrembo
Baraza la Ukunga na Uuguzi Tanzania,
(TNMC)  limeisimamisha kwa muda wa miezi mitatu leseni ya muuguzi,
aliyemchoma sindano ya usingizi na kisha kumbaka kuanzia saa nne usiku
hadi saa nane msichana mwenye umri wa miaka 16, aliyekuwa akimuuguza
mama yake, katika hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
 Baraza la Ukunga na Uuguzi Tanzania  limeviomba vyombo vya ulinzi na
usalama nchini kumkamata popote alipo muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya
Igunga Mkoani Tabora, Damian Mgaya (41) aliyetoroka Hospitalini hapo
kufuatia tuhuma za kumbaka binti huyo wa miaka 16 ili afikishwe kwenye
vyombo vya Sheria.Inaelezwa kuwa mara baada ya kumaliza
kumbaka binti huyo aliamua kumtupa eneo la kufulia nguo kwenye nyasi
akiwa hajitambui na kumwagia maji mwili mzima.
Taarifa hiyo
imetolewa leo Oktoba 18, 2019, na Msajili wa Baraza hilo Agnes Mtawa na
kusema kuwa baada ya mtumishi huyo kurejeshwa kazini, alihamishwa kutoka
kituo cha Afya cha Igurubi na kupelekwa katika hospitali ya Wilaya ya
Igunga.Inaelezwa kuwa muuguzi huyo Damiani Samson Mgaya, mnamo mwaka 2017,
akiwa katika kituo cha Afya cha Igurubi , wilayani humo alishawahi
kufanya tukio kama hilo, ambapo alipelekwa polisi na kisha mahakamani na
hatimae aliachiwa huru na kurejeshwa kazini mwaka 2018.

Kufuatia mtiririko wa matukio hayo kufanywa na muuguzi huyo, Baraza la
Uuguzi na Ukunga Tanzania, (TNMC) limeamua kumchukulia hatua ya
kusimamisha leseni yake ya kutoa huduma za ukunga na uuguzi popote
nchini Tanzania kwa muda wa miezi mitatu.
Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo amethibitisha tuhuma hizo na kusema kesi imefikishwa katika kituo cha polisi.

“Ni kweli tukio lipo na sio mara ya kwanza siku za nyuma Mgaya akiwa
kituo cha afya cha Tarafa ya Igurubi alifanya tukio kama hilo, hii ni
mara ya pili na huu ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu na kanuni za
kiutumishi”- Dkt.Ruta Deus, Mganga Mkuu wa Wilaya.Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *