Mwalimu wa mafunzo ya ndoa, mchungaji peter miti mingi afariki dunia

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema Mchungaji Peter Mingi wa
Kanisa la Ghala la Chakula (Warehouse Christian Centre-WCC) pia
Mkurugenzi wa Voice of Hope Ministry (VHM) inayojihusisha na huduma ya
injili vijijini amefariki dunia usiku huu Jumapili Mei 3,2020.
Baada ya kulitumikia kanisa la TAG kwa miaka mingi kama mchungaji
msaidizi na baadaye kuanzisha huduma ya injili vijijini – VHM, baadaye
Mwalimu na Mchungaji Peter Mitimingi alianzisha kanisa lijulikano kwa
jina la Ghala la chakula au kwa Kiingereza Warehouse Christian Centre –
WCC jijini Dar es salaam.