Mwalimu wa shule ya little treasures afariki kwa kujirusha ghorofani ‘ night club level four’ shinyanga

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao

Na Kadama  Malunde – Malunde 1 blog

Mwalimu wa Shule ya Msingi Little
Treasure iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga,Erick Adams (37) mkazi wa
Bugayambelele amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya nne
ya Night Club ya Level Four Mjini Shinyanga.


Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa
Shinyanga ACP Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea usiku wa
kuamkia leo Jumapili Septemba 22,2019 majira ya saa 12 na dakika 10
katika Jengo Jipya la NSSF ilipo Night Club ya Level Four Shinyanga
Mjini.

“Mwalimu Erick Adams wa Shule ya
Msingi Little Treasure na mkazi wa Bugayambelele alijirusha kutoka
ghorofa ya nne ya Night Club ya Level Four na kufariki dunia akiwa
njiani kupelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kwa matibabu”
,amesema Kamanda Abwao. 

“Chanzo cha tukio hilo
kinachunguzwa.Mbinu iliyotumika ni kujirusha kutoka ghorofa ya Nne
alipokuwa akinywa pombe hadi chini. Mwili wa marehemu umehifadhiwa
hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga ukisubiri kukabidhiwa kwa ndugu”,
ameongeza.
Kamanda Abwao ametoa  wito kwa wamiliki
wa kumbi za starehe zilizopo katika majengo ya ghorofa, kuchukua
tahadhari za kiusalama kwa wateja wao.