Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mwekezaji
kutoka nchini Uturuki, Bw. Mustafa Albayram ameahidi kujenga viwanda
viwili; kiwanda cha nguo na kiwanda cha kutengeneza glasi katika eneo la
Isanga Mjini Bariadi Mkoani Simiyu mwaka 2020, mara baada ya
kuridhishwa na mazingira ya uwekezaji ambapo viwanda hivyo vinatarajia
kuajiri wananchi takribani 2000.

Albayram
ameyasema hayo Novemba 13, 2019 mara baada ya kutembelea maeneo
mbalimbali kwa lengo la kuangalia mazingira wezeshi kwa uwekezaji wa
viwanda, ambaye alifuatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof.
Elizabeth Kiondo kwa ziara ya siku mbili mkoani Simiyu.

Amesema
endapo miundombinu yote muhimu hususani umeme itawekwa kwa wakati
katika eneo hilo uwekezaji huo utaanza mara tu baada ya kukamilisha
taratibu zote muhimu zinazohitajika ikiwa ni pamoja na usajili wa
kampuni na kutafuta hati miliki ya ardhi.

“Tumeamua
kuwekeza Simiyu, kila kitu kikienda sawa kiwanda cha nguo kinaweza
kujengwa na kufanya kazi ndani ya miezi tisa mpaka mwaka mmoja, kiwanda
cha glasi ni mwaka mmoja; baada ya usajili wa kampuni nitarudi tena
Simiyu kukamilisha masuala ya hati miliki ya ardhi, sitaki kumuangusha
Mhe. Balozi maana amefanya mengi kwa ajili yetu,” alisema Albayram.

Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo amesema mwekezaji
ameridhishwa na eneo hilo na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa
kutoa ardhi bure huku akibainisha kuwa ombi kubwa la mwekezaji ni kuwa
na nishati ya kutosha kwa kuwa viwanda hivyo hususani kiwanda cha nguo.

Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemhakikishia
mwekezaji huyo upatikanaji wa mahitaji yote muhimu na kuahidi
kushirikiana na taasisi zote za Serikali zinazohusika kuhakikisha
anapata huduma zote kwa wakati na bila urasimu wowote.

Kuhusu
suala la Umeme Mtaka amesema katika Bajeti ya mwaka 2019/2020 Wizara ya
Nishati kupitia Shirika la umeme TANESCO imetenga fedha kwa ajili ya
ujenzi wa kituo cha kupozea umeme(substation) ambacho kitajengwa karibu
na eneo la uwekezaji huo

Mtaka
ameongeza kuwa mtazamo wa mkoa wa Simiyu ni kuwa na viwanda vichache
vinavyoajiri watu wengi badala ya kuwa na viwanda vingi vinavyoajiri
watu wachache, huku akitoa wito kwa wakulima wa pamba kulima pamba kwa
wingi kwa kuwa kiwanda cha nguo kitakuwa mkombozi wa kuongeza thamani ya
zao la pamba na itauzwa kwa bei ya uhakika.

Naye
Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa pamba nchini, Bw. Boaz Ogola amesema
kujengwa kwa kiwanda cha nguo mkoani Simiyu kutasaidia wakulima wa pamba
kupata soko la uhakika kuondoa changamoto ya bei ya pamba kwa kuwa
kitapanua wigo wa soko la pamba, ambapo pamba inayotumika hapa ni nchini
ni asilimia 20-25 ya pamba yote inayozalishwa.