Mwenyekiti mtaa wa dome bwana najulwa (cheupe) afunga mwaka na mkutano wa hadhara shinyanga

Serikali ya mtaa wa Dome kata ya Ndembezi
Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na wananchi imeendelea kutokumeza
vitendo mbalimbali vya uhalifu ikiwemo wizi na vitendo vya ukatili na kwamba
hatua hiyo imesaidia kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa mtaa
wa Dome Bwana Solomon Nalinga Najulwa leo Disemba 31,2023 kwenye mkutano wa
hadhara wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi kuanzia Mwezi Oktoba
hadi mwezi Disemba Mwaka 2023.

Mwenyekiti huyo amesema ameendelea
kushirikiana na jeshi la polisi akiwemo polisi kata wa kata ya Ndembezi kwa
kushirikiana na wananchi kuzuia uhalifu ambapo pamoja na mambo mengine amesema
serikali ya mtaa huo imefanikiwa kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo ya
kifamilia 26.

“Tumeweza
kusuluhisha migogoro mbalimbali ya kifamilia ipatayo 26 mpaka sasa zinaendelea
vizuri, lakini pia katika kipindi hicho tumeweza kuwaandikia watu 70 barua za
utambulisho wanaoenda maeneo mengine, kuhusu suala la ajira tumewasainia vijana
wa kike na wakiume 22 kupata kazi sehemu mbalimbali, tumewasainia barua za
mikopo jumla ya wakazi 238 wanaume kwa wanawake sehemu mbalimbali za mashirika
kifedha”.

“Katika
suala la miundombinu serikali imeweza kuleta miradi ya barabara katika mtaa
wetu wa Dome jumla ya kilomenta 1.8 zimetengenezwa na wakala wa barabara TARURA
kwa kiwango cha molamu lakini pia kwenye suala la huduma ya afya jumla ya wazee
13 tumewaandikia barua za msamaha wa matibabu kwenye Hospitali yetu ya Mkoa
katika suala la mazingira tumeendelea kutunza bustani kwa kushirikiana na
walengwa wa tasaf tukishirikiana na mzabuni Joseph Kisango katika mradi wa Dome”.

amesema Mwenyekiti Najulwa

“Suala
la ulinzi na usalama tumeendelea kushirikiana na jeshi letu la Polisi chini ya
kamanda Janeth Magomi tumekuwa naye kwa kusaidizana na kijana wake polisi kata
wetu ni askari ambaye ukimpigia simu yuko vizuri usiku na mchana lakini pia
tumeendelea kutokomeza vitendo vyote vya uovu kwa kushirikiana na wananchi
ambapo wanatoa taarifa za viashilikia vya uhalifu mpaka sasa usalama kwenye
mtaa huu ni shwari”.
amesema Mwenyekiti
Najulwa

Polisi jamii wa kata ya Ndembezi Jastin
Nyatano amewataka wananchi kutojihusisha na uhalifu huku akiwakumbusha  kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu
utakaojitokeza hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ya Mwaka mpya ili hatua za
kisheria ziweze kuchukuliwa.

Katika mkutano huo wa hadhara afisa habari
wa jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga Helen Amour ametoa elimu ya
kukabiliana na majanga ya moto huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua
tahadhara ili kuepukana na majanga hao.

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Dome
waliohudhuria mkutano huo wamepongeza kwa juhudi zinazofanywa na serikali hiyo
huku wakishukuru kwa kupata elimu ya kukabiliana na majanga ya moto.


Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Bwana Solomon
Nalinga Najulwa akisoma taarifa ya utekelezaji wa kazi kuanzia Mwezi Oktoba
hadi mwezi Disemba Mwaka 2023.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *