Mwenyekiti wa nccr-mageuzi, james mbatia ashauri muda wa kuchukua fomu serikali za mitaa uongezwe

Mwenyekiti
wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amemtaka Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo
kuongeza muda kuchukua fomu za uchaguzi wa Serikali za mitaa kutokana
na kasoro mbalimbali zilizojitokeza.


Wagombea
wa vyama mbalimbali vya siasa walianza kuchukua na kurejesha fomu
kuwania uwenyekiti wa kijiji, mtaa, kitongoji na ujumbe wa kamati ya
mtaa kuanzia Oktoba 29, 2019. Shughuli hiyo inayofanyika kwa siku saba
itakamilika Novemba 4, 2019.

Akizungumza
mjini Dodoma jana Jumamosi Novemba 2, 2019 Mbatia alisema baadhi ya
maeneo ofisi zilifunguliwa siku mbili tu, baada ya hapo zilifungwa jambo
lililowakosesha  nafasi wagombea wengine kuchukua fomu.

Amesema
Serikali imetoa muda wa siku saba kwa ajili ya wagombea kuchukua na
kurudisha fomu lakini baadhi ya vituo vinafungwa kabla ya muda.

Amesema malalamiko ni mengi kila kona, na kumtaka Jafo kuongeza muda ili wenye nia ya kugombea kujitokeza kwa wingi.