Naibu katibu mkuu mteule ashiriki makabidhiano ya ofisi ya maji mwanza (mwauwasa) na mkurugenzi mpya mteule

Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (aliyekaa kulia) na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza
(MWAUWASA), Mhandisi Leonard Msenyele (kushoto) wakisaini nyaraka za
makabidhiano ya Ofisi. Awali Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji
MWAUWASA. 
Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati kulia) akimkabidhi nyaraka za
makabidhiano ya Ofisi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard
Msenyele (kushoto). Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
MWAUWASA, Christopher Gachuma (wa pili kushoto) na Makamu wake, Edith Mudogo
(wa kwanza kulia
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) mara baada ya
kumkabidhi Ofisi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard
Msenyele. Awali Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA na
Mhandisi Msenyele alikuwa Meneja Miradi MWAUWASA. 
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (aliyekaa) akiwa
katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Gachuma (nyuma
katikati) na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi MWAUWASA mara baada ya kukabidhiwa
rasmi Ofisi.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na wafanyakazi
wa MWAUWASA (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi Ofisi. Wengine katika
picha ni Mwenyekiti wa Bodi, Christopher Gachuma (katikati) na Wajumbe wa Bodi
ya MWAUWASA.
Baadhi
ya wafanyakazi wa MWAUWASA wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji,
Mhandisi Anthony Sanga (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao mara baada ya
kukabidhi Ofisi. Awali Mhandisi Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji MWAUWASA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *