Naibu spika dkt. tulia ackson aongoza semina kuhusu nafasi ya bunge katika mapinduzi ya lishe nchini jijini dodoma

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.
Tulia Ackson (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti
wa Bodi ya Agri Thamani Foundation, Mhe. Mizengo Pinda alipomtembelea
leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.
Tulia Ackson (kushoto) akizungumza na Viongozi  kutoka Agri thamani
Foundation Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Agri Thamani Foundation na Kiongozi wa Msafara,
Mhe. Mizengo Pinda, Mkurugenzi Mtendaji, Ndg. Neema Lugangira (katikati)
na Mwenyekiti wa Kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe, Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dunstan Kitandula (kulia)
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.
Tulia Ackson akiongoza semina kuhusu nafasi ya Bunge katika Mapinduzi ya
Lishe nchini iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Semina hiyo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya
Agri Thamani, Mhe. Mizengo Pinda (kulia kwake), Wajumbe wa Kamati ya
Uongozi ya Bunge, Kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe, Mwenyekiti wa
kamati ya Kudumu ya Bunge ya UKIMWI na Sekretariat ya Kamati ya Uongozi
ya Bunge
Mkurugenzi Idara ya Elimu ya Lishe
kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Ndg. Sikitu Simon
akiwasilisha maada mbele ya Wajumbe Kamati za Kudumu za Bunge za
uongozi, Kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe, Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Wajumbe wa Sekretariat ya Kamati
ya uongozi ya Bunge wakati wa semina kuhusu nafasi ya Bunge katika
Mapinduzi ya Lishe nchini iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini
Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya uongozi, Kikundi cha Wabunge Vinara wa Lishe, Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Wajumbe wa Sekretariat
ya Kamati ya uongozi ya Bunge wakiwa kwenye semina kuhusu nafasi ya
Bunge katika Mapinduzi ya Lishe nchini iliyofanyika leo katika Ofisi za
Bunge Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti
wa Bodi ya Agri Thamani Foundation, Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya uongozi, Kikundi cha Wabunge
Vinara wa Lishe, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya
UKIMWI na Wajumbe wa Sekretariat ya Kamati ya uongozi ya Bunge kwenye
semina kuhusu nafasi ya Bunge katika Mapinduzi ya Lishe nchini
iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti
wa Bodi ya Agri Thamani Foundation, Mhe. Mizengo Pinda akionyesha
kijarida kinachotoa uelewa mpana zaidi wa janga la udumavu na utapiamlo
nchini mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge za uongozi, Kikundi
cha Wabunge Vinara wa Lishe, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Masuala ya UKIMWI na Wajumbe wa Sekretariat ya Kamati ya uongozi ya
Bunge kwenye semina kuhusu nafasi ya Bunge katika Mapinduzi ya Lishe
nchini iliyofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)