Naibu waziri kanyasu asisitiza mahusiano mema kati ya wananchi na hifadhi

Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha
Momella kata ya Ngarenanyuki kuhusiana na mgogoro wa ardhi uliodumu kwa
muda miaka 30 kati ya wananchi hao na Hifadhi ya Taifa ya Arusha ambapo
Mhe. Kanyasu amewataka wahifadhi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia
sheria, Aidha,amewataka wananchi waheshimu sheria za uhifadhi katika
mkutano wa Hadhara uliofanyika leo katika kitongoji Momella mkoani
Arusha.


Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akiwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki,
Dkt. John Pallangyo wakizungumza na Wakuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha
mara baada ya kuwasili katika ofisi za Hifadhi hiyo kabla ya kwenda
kuzungumza na Wananchi wa Kitongoji cha Momella kata ya Ngarenanyuki
wilaya ya Arumeru mkoani Arusha
Mkuu
wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro akizungumza na wananchi wa
Kitongoji cha Momella kata ya Ngarenanyuki kuhusiana na mgogoro wa ardhi
uliodumu kwa muda miaka 30 kati ya wananchi hao na Hifadhi ya Taifa ya
Arusha kabla ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine
Kanyasu kuzungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika
jana katika kitongoji hicho mkoani Arusha.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Dkt.
John Pallangyo akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Momella kata ya
Ngarenanyuki kuhusiana na mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda miaka 30
kati ya wananchi hao na Hifadhi ya Taifa ya Arusha kabla ya Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu kuzungumza na wananchi
hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika kitongoji hicho
mkoani Arusha.
…………………..
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewataka  Watumishi wa Hifadhi ya Taifa
Arusha kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria bila kuwanyanyasa
wananchi.
Aidha, Mhe. Kanyasu amewataka  wananchi kuzingatia sheria za uhifadhi ikiwa pamoja na kushiriki katika kulinda Hifadhi hiyo
 

Ametoa kauli hiyo
leo  wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kitongoji cha  Momela
kata ya Ngarenanyuki katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
 
Hatua hiyo inakuja kufuatia mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda wa miaka 30 baina ya wananchi hao na Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
Wananchi wa Kitongoji
cha Momella wanadai kuwa  mwaka 1992,Hifadhi ya Taifa ya Arusha
ilimega  hekta 600 ya  ardhi ambayo ilikuwa inamilikiwa na Kitongoji
hicho, Licha ya wananchi hao kushinda kesi mahakamani hawajarudishiwa
Ardhi yao hadi leo.
 
Mhe.Kanyasu amewaeleza wananchi hao kuwa
Serikali inautambua mgogoro huo na ni miongoni  mwa  migogoro 1000
inayofanyiwa kazi na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya  Makazi.
 
Kufuatia hali hiyo,
Mhe.Kanyasu amewataka wananchi hao kuendelea kuwa watulivu hadi pale
Serikali itakapotoa orodha ya majina ya vijiji na vitongoji ambavyo
vitakuwa vimeondolewa kwenye Hifadhi nchini.
 
Katika hatua
nyingine, Mhe.Kanyasu amewaatahadharisha wakazi wa Kitongoji hicho
kutokuingiza mifugo ndani ya  Hifadhini kwa kisingizio cha mgogoro huo.
 
Kwa Upande wake
Mbunge wa Arumeru, Dkt.John Pallangyo amewasihi wananchi kuendelea
kuzingatia sheria za Uhifadhi huku wakisubili orodha ya majina ya vijiji
na vitongoji vitakavyotangazwa kuondolewa katika Hifadhi nchini.
 
” Natambua mna
uchungu na mmeteseka kwa muda mrefu juu ya  Mgogoro huu, Niwahakikishie
Waziri kawasikia na kajionea mwenyewe” alisisitiza Mhe.Pallangyo
 
Awali akizungumza
kwenye  mkutano wa hadhara, Mwenyekiti  wa Kitongoji hicho, Anael Nko
amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa kwa muda miaka 30 sasa maisha yao
yameendelea kuwa ya uhasama kati yao na  Hifadhi
 
Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti huyo amemuomba Naibu Waziri  kuumaliza  mgogoro huo kwani umekuwa ukiwarudisha nyuma kimaendeleo 
 
Mbali na hilo,
Mwenyekiti alisema licha ya mgogoro huo wanaihitaji Hifadhi kwa vile
licha ya changamoto hizo wanazokumbana nazo Hifadhi hiyo imekuwa na
manufaa makubwa sana  kwao.