Naibu waziri kigahe atembelea kiwanda cha kuchakata pareto cha pyrethrum company of tanzania ltd (pct) mafinga mkoa wa iringa

 
Naibu
Waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akimsikiliza kwa
makini mtendaji mkuu wa kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum
Company of Tanzania Ltd (PCT) ndugu John Power.

Naibu
Waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akisaini kitabu
cha cha wageni mara baada ya kufika katika kiwanda cha kuchakata pareto
cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT).

Mkuu
wa Wilaya ya Mufindi ndugu Jamhuri Devid Willium akizungumza wakati wa
kikao kilichofanyika katika kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum
Company of Tanzania Ltd (PCT), pembeni ni Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe. Exaud Kigahe.

Mtendaji
mkuu wa kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania
Ltd (PCT) ndugu John Power akizungumza katika kikao kujadili changamoto
za kiwanda, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi ndugu Jamhuri Devid
Willium na aliyekaa katikati ni Naibu Waziri wizara ya Viwanda na
Biashara Mhe. Exaud Kigahe.

Shamba la pareto lililopo katika kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT).

Naibu
Waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akikagua kiwanda
cha kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd
(PCT) kuona uzalishaji wa pareto unaoendelea kiwandani hapo.

Naibu
Waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akiangalia zao
la Sabadilla ambalo linafanyiwa utafiti na kiwanda cha kuchakata pareto
cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT) zao hili linatengeneza
bidhaa zilezile ambazo pareto inatengeneza.

Zao la Sabadilla linalofanyiwa utafiti na kiwanda kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of Tanzania Ltd (PCT).

Na.Mwaandishi wetu,Mafinga

 
Naibu
waziri wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amefanya ziara
ya kutembelea kiwanda cha kuchakata pareto cha Pyrethrum Company of
Tanzania Ltd (PCT) kilichopo Mafinga Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa
na kujionea shughuli za kiwanda zikiendelea za uchakati wa pareto.
Mhe.
Kigahe amefanya ziara hiyo leo tarehe 24 Aprili, 2021 katika kiwanda
hicho chenye uwezo wa kuzalisha tani 5000 kwa mwaka ambapo uzalishaji
wake kwa sasa ni tani 300 na hii imetokana na changamoto ya upatikanaji
wa malighafi ambayo ni pareto. 

Kiwanda cha PCT kwa sasa
kimeajiri wafanyakazi wa kudumu 146 na wafanyakazi wasio wa kudumu wako
zaidi ya 100 ambapo masoko ya kiwanda hiki kwa kiasi kikubwa zaidi ya
asilimia 90 wanauza nchini Marekani ndipo kuna soko kubwa, masoko
mengine ni Japan na India. 

“lengo la ziara yangu ni
kutembelea kiwanda hiki na kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo
ili kuhakikisha zinatatuliwa kwa wakati na kutoa fursa kwa wakulima
kulima kwa kiasi kikubwa kwani soko lipo katika kiwanda hiki, serikali
inahitaji kiwanda hiki kiongeze uzalishaji ili kuongeza ajira na kodi
kwa serikali lakini pia kipato cha mwananchi mmoja mmoja”amesema Mhe.
Kigahe. 

Mhe. Kigahe ameongeza kuwa serikali inahitaji kuwa na
viwanda vingi vinavyochakata mazao ya kilimo na kuongeza thamani kabla
ya kuuza nje ya nchi ili kuongeza fedha za kigeni na kukuza pato la
taifa hivyo mkazo mkubwa ni katika kuhakikisha serikali inalinda viwanda
vya ndani hasa vinavyochakata mazao ya kilimo. 

Mkuu wa
Wilaya ya Mufindi ndugu Jamhuri Devid Willium amempongeza Mhe. Naibu
waziri kwa kutembelea kiwanda hicho kwani kiwanda hiki kina historia
kubwa ya nchi yetu, wakulima wa Mufindi ni wakulima wazuri wa pareto kwa
kutumia vyama vya ushirika AMCOS ambao wanasaidia pia katika
upatikanaji wa pembejeo. 

Mhe. Jamhuri amesema kuwa walanguzi
wa zao la pareto wamekuwa wakidhibitiwa kwa nguvu zote katika wilaya ya
Mufindi kwani walanguzi hao wanakwepa kodi, wanawapunja wakulima katika
mizani, hawalipi kodi ya halmashauri na serikali ya wilaya. 

Juhudi
kubwa zimekuwa zikifanywa na kiwanda cha PCT ya kutoa mbegu bora bure
kwa wakulima, kutoa mafunzo ya kilimo bora na vikaushio vya pareto
katika kurahisisha kukausha pareto, bado kumekuwa na changamoto kwa
wakulima kutokuwekeza katika kilimo cha pareto. 

Kiwanda cha
PCT kipo katika mpango wa kuanzisha kilimo cha kisasa cha (Block
farming) ambayo itakuwa suluhisho kwa wakulima kulima shamba kubwa
wakisaidiwa pembejeo na vitendea kazi pamoja na huduma nyinginezo za
ugani. 

Mhe. Exaud Kigahe ametembelea pia shamba la zao la
SABADILLA ambalo bado liko katika utafiti kwa mwaka wa nne sasa na
karibu itatolewa tathimini ya utafiti huo ambapo zao hili litasaidia
kuongeza mazao mengine mbadala ili kutoa fursa kwa wakulima kulima mazao
mengine kwa gharama nafuu zaidi.

 Zao la SABADILLA ni zao ambalo linatengeneza bidhaa zilezile ambazo pareto inatengeneza. 

Kwa
upande wake Mhasibu Mkuu wa kiwanda cha PCT ndugu Gerald Joseph
ameshukuru sana kwa ujio wa Mhe. Naibu waziri kwani wamepata fursa ya
kutosha kueleza changamoto zao na waziri amehaidi kuzifanyia kazi kwa
haraka katika kusaidia kuongeza uzalishaji wa pareto ili kuhamasisha
wakulima kuongeza ulimaji wa pareto.