Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe,akizungumza na wadau
wa Sekta ya Nguo na Mavazi alipokutana nao ili kisikiliza changamoto
wanazokutana nazo katika uendelezaji wa Viwanda na biashara ya nguo na
mavazi nchini jijini Dodoma
Katibu
wa Jumuiya ya Wafanyabishara Tanzania (JWT) Bw. Abdala Mwinyi
akiwasilisha changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa nguo na mavazi
hususan vitenge kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud
Kigahe(MB) katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma
Wadau
wa sekta ya nguo na mavazi wakiwa katika kikao cha pamoja na Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, chenye lengo la
kisikiliza na kutatua changamoto wanazokutana nazo katika uendelezaji wa
Viwanda na biashara ya nguo na mavazi nchinikilichofanyika jijini
Dodoma
Katibu
Mtendaji wa Chama cha Wazalishaji Nguo na Mavazi Tanzania TEGAMAT
akiwasilisha changamoto zinazowakabili wanachama wake kwa Naibu Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe(MB) alipokutana na wadau wa
Sekta ya Nguo na Mavazi ili kisikiliza changamoto wanazokutana nazo
katika uendelezaji wa Viwanda na biashara ya nguo na mavazi nchini
kilichofanyika jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, akifafanua jambo kwa
wazalishaji na waagizaji wa nguo na mavazi hususani vitenge na kanga
katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma
Baadhi
ya Waagizaji wa nguo na mavazi hususan vitenge kutoka nje ya nchi
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe(MB)
(hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amekutana na kufanya
mazungumzo na wadau wa sekta ya nguo na mavazi ili kusikiliza changamoto
wanazokutana nazo na mapendekezo yao katika kuboresha na kukuza sekta
hiyo.
Akizungumza na wadau hao katika kikao kilichofanyika leo tarehe 9
Februari 2021 jijini Dodoma Mhe Kigahe aliwaagiza kuwasilisha
changamoto walizonazo na rasimu za mipango mikakati ya kuboresha na
kuendeleza Viwanda na Biashara katika sekta hiyo ili kukuza uchumi wa
nchi.
Aidha
katika kikao hicho kilichojumuisha wadau ambao ni watengenezaji na
waagizaji wa nguo na mavazi kutoka nje ya nchi, wadau hao waliwasilisha
changamoto na mapendekezo yao kwa Mhe. Naibu Waziri wakiwa na lengo la
kuboresha na kukuza sekta hiyo.
Aidha,
Mhe.Kigahe amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali
katika kuendeleza sekta ya nguo na mavazi nchini ikiwemo kukuza soko la
ndani la bidhaa.
Aidha
amesema kuwa amekuwa wakianda na kutekeleza Mkakati wa kuendeleza
Sekta ya pamba nguo hadi mavazi ( Cotton to Clothing Strategy C2C 2016 –
2020 ) na kuuhuisha ambapo utekelezaji wake utaanza mwaka 2021 – 2032.