Ndege ya pili boeing 787-8 dreamliner yaondoka marekani….kutua nchini leo mchana

Ndege
mpya ya pili aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na Serikali
kwa ajili ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeondoka nchini Marekani
jana Ijumaa, Oktoba 25, 2919 kuja Dar es Salaam Tanzania.


Ndege
hiyo kubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 inatarajiwa kutua katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo
mchana Oktoba 26, 2019.

Ndege hiyo itapokelewa na wananchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Hii
inakuwa ndege ya 8 kati ya ndege 11 zilizonunuliwa na Serikali kwa
lengo la kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kukuza utalii na
uchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *