Nhif yawataka waandishi wa habari nchini kujiunga uanachama na klabu za waandishi wa habari ili wapate huduma za bima

Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Shedrack Mapunda akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha kuhusu kuanzishwa kwa vifurushiv vipya vya bima ya afya nchini kupitia mfuko huo
Meneja wa Mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Arusha NHIF, Isaya Shekifu
Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu akizungumza kwenye kikao cha Mkurugenzi wa NHIF na Waandishi wa habari
waandishi wa habari Mkoa wa Arusha wakiwa ukumbini wakisubiri kuanza kwa kikao na Mkurugenzi wa NHIF
waandishi wa habari wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa(mtoa mada hayupo pichani)
waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Baadhi ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Shedrack Mapunda wa nne kutoka kushoto aliyekaa pamoja na viongozi wengine wa mfuko huo

Na Seif Mangwangi, Arusha 
WAANDISHI wa habari nchini,
wametakiwa kujiunga uanachama katika klabu za waandishi wa habari (Press Clubs), katika Mikoa yao
ili waweze kupata fursa ya kuungwa kwenye huduma ya bima ya afya inayotolewa
kupitia mfumo wa vikundi.
Akizungumza kwenye kikao cha pamoja
na waandishi wa habari Mkoa wa Arusha kwa lengo la kuwaeleza vifurushi vipya
vilivyoanzishwa na taasisi hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Christopher
Mapunda amesema kutokana na kuanzishwa kwa vifurushi vipya waandishi wa habari
watatakiwa kujiunga na Klabu za waandishi wa habari ili wapate huduma kupitia bima ya afya.
Pia mesema baada ya kufanya tathmini
ya muda mrefu ya maendeleo ya mfuko wa bima ya afya nchini, wamekuja na mfumo
mpya ambapo utawezesha mtu mmoja mmoja kujiunga kwa gharama nafuu kulingana na
vifurushi vilivyopo huku waandishi wa habari wakiangukia katika kundi la Umoja.
“Zamani mtu mmoja alitakiwa kulipa
gharama ya Tsh 1500,000 fedha ambayo ilionekana kuwa kubwa sana lakini kwa
mfumo huu mpya kila mtu atajipimia kadiri anavyoona anaweza na kulipia na
kupata huduma,”amesema.
Amevitaja vifurushi hivyo kuwa ni
pamoja na Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya ambapo kwa kifurushi cha
Najali mtu mmoja gharama yake ya chini ya Tsh192,000 kwa mtu mwenye umri wa
miaka 18-35, wenye umri wa miaka 36-59 watalipita 240,000 na kwa wenye umri
zaidi ya miaka 60, watalipia Tsh360,000.
 “Waandishi wa habari wao wako kwenye kikundi
cha Umoja ambapo kupitia mfumo huu waandishi wa habari watatakiwa kulipia laki
moja (Tsh 100,000/-), lakini akitaka kumuingiza mwenzi wake atapaswa kumlipia
kiasi kingine kama hicho na watapata huduma katika hospitali zote ambazo NHIF
imeingia nazo mkataba,”amesema.
Amesema kwa watakaojiunga na mfumo
wa jipimie, watatakiwa kupata huduma katika hospitali na vituo vyote vya Afya
katika Mkoa na kama maradhi watakayotibiwa yatahitaji rufaa watapewa rufaa
katika hospitali kubwa za rufaa katika Mikoa, Kanda na hata Taifa.
Aidha amesema waandishi wa habari  kuendelea kuchangiana kwa ajili ya ugonjwa sio
sawa kwa kuwa sio kila wakati wanaokuchangia wanakuwa na fedha jambo ambalo
linaweza likasababisha maradhi kuendelea kuwa makubwa.
Kwa upande wake Meneja wa NHIF Mkoa
wa Arusha Isaya Shekifu amesema amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha waandishi
wa habari wanapata huduma ya  bima ya
afya kwa kuwa ni watu muhimu katika jamii na kuwataka kufika ofisini kwake
kwaajili ya kufanya mazungumzo ya namna ya kuendeleza huduma hiyo Mkoani
Arusha.
Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu
amewataka waandishi wa Habari Mkmoa wa Arusha kutumia nafasi hiyo ya upendeleo
kujiiunga na Chama ili kupata bima na kuondokana na adha mbalimbali wanazopata
pindi wanapougua kwa kukosa huduma ya bima kwaajili ya matibabu.
Amesema ijapokuwa kujiunga na klabu
za waandishi wa habari ni jambo la hiyari lakini ugonjwa unapomfika mtu yoyote
sio jambo la hiyari katika kuupatia tiba hivyo ni vyema kama watajiunga na APC
ili waweze kupata fursa ya kupata bima.
Pia amesema APC imeshakusanya fedha
za wanachama wake kwaajili ya kupata huduma ya bima ya afya na hivyo baada ya
kikao hicho uongozi utakutana na maafisa wa NHIF Mkoa wa Arusha na kupitia
vigezo vinavyohitajika ili waweze kuanza kupata huduma.