Nyongo ataka wafanyabiashara wa madini wasikamatwe kamatwe hovyo

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi
mkoani hapa Zelothe Stephen akihutubia kwenye mkutano wa mabalozi wa Tanzania
na China kuelezea fursa za kibiashara kwa wafanyabiashara wa sekta ya madini
mkoani Arusha kwenye ukumbi wa Hotel ya Mount meru jijini Arusha picha na Ahmed
Mahmoud Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
akiwa Ofisini kwake  na mgeni wake Balozi
wa China nchini Tanzania Wang Ke wakizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano
kwenye Nyanja mbalimbali za kibiashara na maendeleo jijini Arusha picha na Ahmed
Mahmoud Arusha
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi
mkoa wa Arusha Zelothe Stephen akibadilisha mazungumzo na Balozi wa China
nchini Wang Ke kwenye Ofisi za Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kabla ya
Balozi huyo kufanya ziara chuo cha Uhasibu Arusha na baadae kwenye mkutano na
wafanyabiashara wa sekta ya madini jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Sehemu ya wafanyabiashara wa sekta
ya madini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tamida Sammy Mollel wakimsikiliza Naibu
waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati akifungua mkutano huo wa siku moja
kwenye ukumbi wa hotel ya Mount Meru jijini Arusha leo picha na Ahmed Mahmoud Arusha
Naibu waziri wa Madini Stanslaus
Nyongo akifungua mkutano wa wafanyabiashara wa sekta ya madini kwa ajili ya
kutangaza Fursa za kibiashara kwenye sekta ya madini na kuitangaza fursa za
sekta hiyo zinazopatikana nchini kwa ujumbe wa Balozi wa China kwenye ukumbi wa
hotel ya Mount Meru Jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha
Na Ahmed Mahmoud,Arusha
NAIBU Waziri wa
Madini Ladslausi Nyongo  amepiga marufuku tabia ya  kamatakamata ya 
 wafanyabiashara wa madini nchini waliohifadhi  madini maeneo 
wanayotaka kwa mujibu wa sheria.
Aidha katika
kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 Mkoa wa Arusha umekusanya  zaidi ya
Sh.bilioni  30 zinazotokana na madini ya Vito ya aina mbalimbali.
Akizungumza
jana Jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa Mabalozi wa China nchini
Tanzania na Tanzania nchini China pamoja na wafanyabiashara wa madini
nchini,Naibu Waziri Nyongo alisema sheria inaruhusu wafanyabiashara
kukaa na madini ili mradi wafuate sheria.
“Lakini
siku za karibuni kumezuka tabia ya kusumbua wafanyabiashara waliofuata
sheria za kukaa na  madini kwa kulipa kodi zote wanazotakiwa ili wakauze
mahali popote wanapotaka,lakini wanasumbuliwa kwa kukamatwa na vyombo
vya ulinzi,”alisema.
Alisema ili kuondoa
mkanganyiko huo Wizara imejipanga kuelemisha wadau wa madini vikiwemo
vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu sheria za madini ikiwemo inayoruhusu
wafanyabiashara hao kushikilia madini kabla ya kuuza kwenye soko za
madini zilizopo.
Aidha aliomba Mabalozi wa
China nchini Tanzania na yule wa Tanzania nchini China kuja kuwekeza
nchini kwenye uwekezaji wa uongezaji thamani masini chini ya Gramu mbili
ambayo yanaruhusiwa kwenda nje ya  nchi bila kuonhezwa thamani.
“Kama mnateknolojia ya kuongeza thamani madini haya tunawaalika mje kuwekeza ili tusiyatoe nje bila kuongeza thamani,”alisema.
Mkuu
wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo alisema wameleta mkutano huo ili kuongeza
fursa kwa wafanyabiashara katika kupanua wigo wa soko la madini.
Alisema
nchi ya Tanzania ina madini mengi lakini mchango wake kwa pato la Taifa
ni asilimia 5.07 tofauti na pato la sekta ya utalii asilimia  17 na
asilimia 25 katika kuingizia Taifa fedha za kigeni.
“Mchango
huu hautoshi hivyo tumeamua kutumia mkutano huu ili tuongeze fursa
katika madini na kukuza zaidi pato la sekta hii,”alisema.
Kuhusu
ukusanyaji wa madini alisema yanatokana na soko la madini Namanga
kukusanya Sh.bilioni 1.7  ya  madini ya vito na soko la Arusha
walikusanya Sh.bilioni 34.46 katika kipindi cha Juni 2019 hadi Desemba
2019.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof.Idrisa
Kikula aliomba  Ofisa Madini Mkazi wa Mikoa yote kukaa pamoja na vyombo
vya ulinzi na usalama kuelimishana sheria za madini ili wafahamu jinsi
ya kudhibiti utoroshaji wa madini.
Balozi wa
Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliomba wafanyabiashara kutumia
fursa ya mkutano huo kuongeza mapato ya madini kutoka Sh.bilioni 500 ya
sasa hadi kufikia Sh.Trioni moja.
“China
wanunuzi wakubwa wa dhahabu  kama mwaka jana 2019 walinunua dhahabu tani
1506 hiki sio kiwango kidogo na hata madini mengine wananunua sana
hivyo tujitahidi kuongeza fursa za soko nchini China,”alisema.