Ofisi ya makamu wa rais kwa kushirikiana na wizara ya viwanda na biashara yakutana na wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa mifuko mbadala wa plastiki

Ofisi
ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara
imeandaa kikao kilichowakutanisha Wazalishaji, Wauzaji na Wasambazaji wa
mifuko mbadala wa plastiki. 


Kikao
hiko kimefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Kmbarage Nyerere
(JNICC) jijini Dar Es Salaama Lengo la Kikao hiko ni kusikiliza hoja na
changamoto mbalimbali kutoka kwa Wazalishaji, Wauzaji na Wasambazaji wa
mifuko hiyo, na hivyo basi kuwezesha Serikali kuzipatia changamoto hizo
uvumbuzi.

Akiongea
katika Kikao hiko Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda kutoka
Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Leo Lyayuka alisema kuwa zoezi zima la
upigaji marufuku mifuko ya plastiki limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na
lilifanyika kwa weledi hali iliyopelekea kutokua na malalamiko yoyote
kutoka kwa wananchi.

“Kwenye
mafanikio yoyote hapakosi changamoto, vivohivyo, kwenye zoezi hili,
ingawa tumepata mafanikio makubwa lakini kuna changamoto ambazo
zimejitokeza na kama zisipotafutiwa ufumbuzi wa haraka zitaharibu na
kurudisha nyuma mafanikio makubwa yaliyopatikana. Kwahiyo kikao chetu
kitajikita katika kuzibaini changamoto zote na kupendekeza mapendekezo
namna ya kutatua”.Alisema Bwana Lyayuka.

Naye
Mkurugenzi Msaidizi toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Kemilembe Mutasa
alisema kuwa Kikao hiko kina lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu
utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki, kuibua changamoto za
utekelezaji na namna ya kukabiliana na changamoto husika hususani katika
masuala yafuatayo:- Viwango vya ubora vinavyotakiwa vya mifuko mbadala
wa plastiki, Hali ya uzalishaji na usambazaji wa mifuko mbadala wa
plastiki, Uzalishaji na upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya mifuko
mbadala wa plastiki, Viwango vya ubora wa mifuko mbadala na Changamoto
zinazojitokeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki.

Ofisi
ya Makamu wa Rais imekua ikiandaa vikao kama hivyo mara nyingi ili
kuweza kupata maoni na changamoto juu ya uzalishaji, usambazaji na
biashara ya mifuko mbadala wa plastiki kwa pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *