Ombaomba mbeya waonywa kutembea na kundi la watoto wanapoomba mitaani

Na Joachim Nyambo,Mbeya.
OMBAOMBA MAARUFU JIJINI MBEYA ANUSURIKA KICHAPO MARA BAADA YA ...
Ombaomba Mkoani Mbeya
SHIRIKISHO
la Vyama vya watu wenye ulemavu mkoani Mbeya limekemea vikali tabia ya
baadhi ya walemavu kutumia mwanya wa watoto kutokwenda shule kutokana na
Ugongwa wa Homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona
kuwatumikisha kwa kuongozana nao mitaani wanakofanya shughuli za
ombaomba.
Tangu
Serikali ifanye uamuzi wa kufunga shule kuanzia za
Awali,Msingi,Sekondari na vyuo hapa mchini,na kuwataka wanafunzi kubaki
majumbani mwao ikiwa ni njia mojawapo ya kuepuka mikusanyiko isiyo ya
lazima,mkoani Mbeya kwa upande wa wazazi wanaofanya shughuli za ombaomba
wanaonekana kuitumia vibaya fursa hiyo kwa kuzurula na watoto wao.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi Ofisini kwake,Katibu wa Shirikisho la Vyama
vya watu wenye ulemavu mkoani hapa,Jimmy Ambilikile alisema
kinachofanywa na wazazi hao ni jambo linalohatarisha maisha ya watoto
wao.
Ambilikile
alisema kama Shirikisho wamefuatilia kwa karibu na kushuhudia mara
kadha wazazi na walezi wanaofanya shughuli za ombaomba hasa kwenye
maeneo ya biashara wakiongozana na watoto wao pasipo kujali tahadhali
zinazotolewa na Serikali na wadau wengine wa Sekta ya Afya.
Alisema
hatari zaidi inakuja pale ambapo ombaomba hao ambao wengi wao ni wale
wasioona hawaishii kuongozana na mtoto mmoja kwaajili ya kumuongoza bali
huongozana na watoto wa familia yake yote hasa walio wadogo jambo
alilosema tayari wanakuwa wamesababisha mkusanyiko mwingine.
Ambilikile
ambaye pia ndiye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha walemavu(Chawata)
nchini na pia Mwenyekiti wa Chama chama hicho mkoa wa Mbeya alisema ni
vema wazazi na walezi wakafuata utaratibu uliopangwa na Serikali wa
watoto kubaki majumbani na kama wanahitaji wasaidizi basi watembee na
mtoto mmoja na si kundi la wanafamilia kama inavyofanyika sasa.
“Utakuta
mlemavu mmoja ameongozana na watoto watatu wane mpaka watano..hao
wanatembea..bado kuna mdogo aliyembeba mgongoni sasa wanapoingia eneo la
biashara kama dukani kuomba wakakutana na watoa huduma na wateja tayari
huo ni mkusanyiko wenye hatari katika kipindi hiki.Haya watoto wenyewe
kutokana na umri mdogo karibia kila eneo wanalopita wanataka kushika
vitu watafungua milango na kumbuka wakipewa msaada wa vitu wanavishika
na kunawakati hawanawi mikono yao..Sasa unaweza kuona mnyororo wa
maambukizi unavyoweza kutokea iwapo katika moja ya maeneo waliyopita
kuna Virusi vya Corona.”alifafanua Ambilikile.
Katibu
huyo aliwataka walemavu wanaofanya shughuli za ombaomba kutambua kuwa
kipindi hiki cha Mapambano dhidi ya Corona ni hatari na kinahitaji
umakini mkubwa kwa kufuata maelekezo yanayotolewa kila wakati.
Alisema
kuachana na mazoea kutaiwezesha jamii kuwa salama na hatimaye kuivusha
katika kipindi kigumu kinachoendelea alichosema kila mmoja anapaswa kwa
nafasi yake kujiuliza anafanya nini kujikinga yeye,familia yake na jamii
inayomzunguka.