Picha: rais magufuli akutana na kufanya mazungumzo na maalim seif sharif hamad ikulu jijini dar

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT
Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad kwa kutokugusana mikono, Ikulu
Jijini Dar es Salaam. Salamu hiyo ya kutokugusana mikono ni kutekeleza
ushauri ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu wenye lengo kujihadhari dhidi ya virusi vya ugonjwa wa
Corona.


Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika mazungumzo ya faragha na Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni
Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad, Ikulu
Jijini Dar es Salaam.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana Mwanasiasa Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa Chama cha ACT
Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
Ikulu Jijini Dar es Salaam.