Picha : rais magufuli amuapisha cag mpya…je charles kichere ni nani??


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Bw. Charles
Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (
Controller and Auditor General – CAG). Hafla
iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi
vitendea kazi
Bw.
Charles Edward Kichere mara baada ya kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (
Controller
and Auditor General – CAG
).
Hafla iliyofanyika Ikulu jijini dar es salaam Novemba 4, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe.
Job Ndugai, Jaji Mkuu Mhe. Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Dkt. John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Agustine Mahiga, Waziri wa
Mambo ya Nje Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Fedha Dkt. Isidori Mpango  pamoja na
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (
Controller and Auditor General
– CAG)
,
Majaji 12 wa Mahakama kuu,
Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu
Tawala wa Mkoa wa Njombe,

Balozi wa Tanzania Nchni Kuwait pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala Bora mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam novemba 4,
2019.
 **


Charles Kichere ni nani?

Alisomea elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam na chuo kikuu cha Tumaini, Jijini Dar es Salaam.

Kichere aliwahi kuwa naibu kamishna mkuu wa TRA.

Mnamo tarehe 25 Machi mwaka 2017, aliteuliwa na rais Magufuli kuwa kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).

Aliipokea nafasi hiyo kutoka kwa Alphayo Kidata ambaye aliteuliwa wakati huo kuwa katibu mkuu ikulu Tanzania.

Charles Kichere alihudumu kama kamishna
wa TRA kuanzia Machi 2017 hadi Juni mwaka huu 2019, wakati aliondoshwa
katika mamlaka hiyo ya TRA, katika mageuzi ya rais Magufuli aliyotoa
ikulu mjini Dar es Salaam kupitia taarifa rasmi ya mkurugenzi wa
mawasiliano ya rais.

Kichere aliteuliwa badala yake kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.

Yuko kwenye bodi ya Benki ya CRDB Tanzania.

Zamani alikuwa mkaguzi mkuu wa shirika
la Kitaifa la barabara, mweka hazina na pia mkaguzi mkuu wa hesabu
katika kampuni ya majani chai ya Unilever nchini Kenya na Tanzania.

Amepokea wadhifa wa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali kutoka wa Profesa Mussa Assad.

Orodha ya wadhibiti na wakaguzi wa hesabu za serikali Tanzania

Bwana. R.W.A. McColl aliyehudumu 1961 hadi 1963 
Bwana. Gordon. A. Hutchinson aliyehudumu 1964 hadi 1969 
Bwana. Mohamed Aboud aliyehudumu 1969 hadi 1996 
Bwana. Thomas Kiama aliyehudumu 1996 hadi 2005 
Mr. Ludovick S. L. Utouh aliyehudumu 2006 hadi 2014 
Prof. Mussa Juma Assad aliyehudumu 2014 hadi 2019 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *