Polisi tabora kuanza msako wa wanaotaka kujinyonga 2020….”tutawakamata kabla hawajajinyonga”

Baada
ya kupokea taarifa ya Watu wawili kujinyonga mpaka kupoteza maisha
Tabora, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa amesema
Polisi wataanza msako wa kuwabaini na kuwakamata wote wanaotarajia
kujinyonga mwaka huu na kuwapelekea Mahakamani.Kwa
mujibu wa RPC Mwakalukwa, walijionyonga ni  Mwalimu Basil Sungu (39) wa
shule ya msingi Ikongolo Wilaya ya Uyui mkoani Tabora ambaye 
amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kipande cha kitenge cha mke wake.

Amesema mwili wa Sungu ulikutwa chumbani kwake ukiwa unaning’inia darini Jumanne iliyopita ya Desemba 31, 2019.


Mwingine
ni James Albert (22), mjasiriamali na mkazi wa kata ya Chemchem
Manispaa ya Tabora ambaye amekutwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia
mkanda wa begi.
“Niwambie
mwaka huu tabia hizo zikome kwa wanaotegemea kujinyonga tutaanzisha
doria kuhakikisha wote wanaotarajia kujinyonga mwaka huu tunawakamata
kabla hawajinyonga na tunawapelekea mahakamani”
Amesema RPC  Mwakalukwa huku akisema uchunguzi dhidi ya matukio haya mawili unaendelea ili kujua chanzoLeave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *