Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole
Gabriel,akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya
uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni,
Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole
Gabriel,akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni
ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni,
Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Sehemu
ywa wafugaji wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa
awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika
kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi, Dk.Fatuma Mganga,akizungumza kwenye
uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika
leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu
wa Wafugaji Kata ya Bahi Bw.Yona Paulo ,akitoa neno wakati wa uzinduzi
wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika
kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Bahi,Jeremiah Mapogo,akizungumza katika uzinduzi wa
awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika
kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi
wa Huduma za Mifugo, Dk.Hezron Nonga,akitoa takwimu wakati wa uzinduzi
wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika
kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Mkuu
wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Daniel Kehogo, akisoma taarifa ya
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Prof.Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa awamu
ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji
cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akipokea
taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya
Mifugo na Uvuvi Bw.Daniel Kehogo wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya
kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi
Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akigawa
dawa za Kuogesha mifugo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi,
Dk.Fatuma Mganga pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bahi,Jeremiah
Mapogo wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji
mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi,
Mkoa wa Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji
mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi,
Mkoa wa Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akimswaga
ng’ombe kuingia kwenye maji tayari kwa ajili kuoga dawa baada ya
uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika
leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akikagua
mifugo mara baada ya kuzindua awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji
mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi,
Mkoa wa Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akiangalia
Dume la Ng’ombe baada ya kuzindua awamu ya tatu ya kampeni ya
uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni,
Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua awamu ya tatu ya kampeni
ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni,
Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
…………………………………………………………………………………………….
Na Alex Sonna, Bahi
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel, leo
amezindua awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo, huku akiwataka
wafugaji nchini kuhakikisha wanaogesha mifugo ili kudhibiti magonjwa
yanayoenezwa na kupe.
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani
Bahi, Mkoa wa Dodoma, Prof.Elisante amesema lengo la serikali ni
kuongeza toja ya ufugaji kwa kuwa na mifugo yenye afya itakayozalisha
mazao zaidi yenye ubora wa kitaifa na kimataifa.
“Lengo
la kuogesha mifugo ni kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na kupe hususan
Ndigana kali ambayo imekuwa ni changamoto katika kuendeleza tasnia ya
mifugo nchini,”amesema.
Amebainisha kuwa magonjwa hayo yamekuwa yakiathiri mifugo na kusababisha hasara kubwa kwa mfugaji.
“Magonjwa
yanayoenezwa na kupe yasipodhibitiwa ipasavyo huchangia asilimia 72 ya
vifo vyote vya ng’ombe nchini, kati ya magonjwa hayo, ugonjwa wa Ndigana
kali huchangia vifo kwa kiwango kikubwa cha asilimia 44,”amesema.
Katibu
Mkuu huyo amesema hasara inayotokana na magonjwa hayo inakadiriwa kuwa
takribani Sh.Bilioni 145, na kusababisha kupungua uzalishaji maziwa,
nyama kutokana na kukonda, kushuka kwa thamani ya ngozi, kupoteza
wanyama kazi na udumavu wa ndama.
Amefafanua
kuwa uogeshaji wa mifugo kwa kutumia josho ni mzuri na hasa kwa
wafugaji wenye mifugo mingi na unadhibiti magonjwa hayo.
Amesema
mwaka 2018 Wizara hiyo ilitengeneza mkakati wa kudhibiti magonjwa hayo
kwa kuanzisha kampeni hiyo ambapo kwa awamu ya kwanza na pili serikali
ilinunua lita 21,373.06 zenye thamani ya Sh.Milioni 740.7 kwa ajili ya
kuogesha mifugo.
“Katika
awamu zote mbili kumekuwa na jumla ya michovyo Milioni 245.37 ya mifugo
yote ikiwemo ng’ombe Milioni 176.32, Mbuzi Milioni 58.02, kondoa
Milioni 20.03 na punda 2,685,”amesema.
Kuhusu
kampeni huyo awamu ya tatu, amesema serikali imenunua dawa ya kuogesha
mifugo aina ya Paranex, Paratop, Amitraz kiasi cha lita 15,579 zenye
thamani ya Sh.Milioni 592.82 ambazo zitatosheleza majosho 1,983 katika
halmashauri 162 na michovyo inayotarajiwa ni Milioni 405 ya mifugo yote
itakayoogeshwa.
Ameagiza
Halmashauri kusimamia kanuni ya uogeshaji ili wafugaji waifuate na
kushirikiana nao na wadau kujenga na kukarabati majosho yake na
miundombinu mingine ya mifugo.
Awali,
akitoa taarifa ya uogeshaji mifugo wilayani Bahi, Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya hiyo, Dk.Fatuma Mganga, amesema mifugo inachangia
zaidi ya asilimia 55 ya mapato ndani ya Halmashauri hiyo kwa mwaka.
Amesema kuna minada 15 ambayo hufanyika biashara ya kuuza wastani wa ng’ombe 3,882, mbuzi 4,602 na kondoo 89 kwa mwezi.
Hata
hivyo, amesema halmashuari imekwisha andika andiko la mradi wa kiwanda
cha uchakataji ngozi lenye thamani ya Sh.Bilioni 3.3 tayari andiko hilo
lipo Wizara ya Fedha kwa ajili ya mapitio ya mwisho kabla fedha
kutolewa.
Naye,
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Dk.Hezron Nonga, amesema mwaka 2019,
majosho zaidi ya 511 yalikarabatiwa nchi nzima kwenye Halmashauri huku
78 mapya yalijengwa.
“Vifo
vya ng’ombe hususan ndama vilipungua kwa asilimia 30 kwasababu ya
uogeshaji, tukiogesha vifo vya ng’ombe zetu tunatokomeza,”amesema.