Prof.mchome asisitiza uwazi na ushirikishwaji katika utendaji ofisi ya wakili mkuu wa serikali

 

Katibu
Mkuu Wizara ya Katiba na sheria Prof. Sifuni Mchome ,akizungumza wakati
akifungua Kikao cha pili cha Baraza la wafanyakazi wa ofisi ya wakili
Mkuu wa Serikali unaofanyika Leo April 9,2021 jijini Dodoma,kushoto
kwake ni Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata na kushoto ni Naibu
Wakili Mkuu wa Serikali Bw.Boniphance Luhende.



Wakili
Mkuu wa Serikali Gabriel Malata,akitoa utangulizi wa ufunguzi wa Kikao
cha pili cha Baraza la wafanyakazi wa ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali
unaofanyika leo April 9,2021 jijini Dodoma (katikati) ni Katibu Mkuu
Wizara ya Katiba na sheria Prof. Sifuni Mchome na kulia ni Naibu Wakili
Mkuu wa Serikali Bw.Boniphance Luhende.



Mwenyekiti
wa TUGHE Tawi la Wakili Mkuu wa Serikali Bw.Mtani Songorwa ,akitoa neno
la shukrani kwa niaba ya washiriki mara baada ya Katibu Mkuu Wizara ya
Katiba na sheria Prof. Sifuni Mchome,kufungua Kikao cha pili cha Baraza
la wafanyakazi wa ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali kilichofanyika Leo
April 9,2021 jijini Dodoma.



Baadhi
ya washiriki wa kikao hicho wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba
na sheria Prof. Sifuni Mchome (hayupo pichani) wakati akifungua Kikao
cha pili cha Baraza la wafanyakazi wa ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali
kilichofanyika Leo April 9,2021 jijini Dodoma.



Katibu
Mkuu Wizara ya Katiba na sheria Prof. Sifuni Mchome akiwa katika picha
ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua Kikao cha pili cha Baraza
la wafanyakazi wa ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali kinachofanyika Leo
April 9,2021 jijini Dodoma.




Na.Alex Sonna,Dodoma


Katibu
Mkuu Wizara ya Katiba na sheria Prof. Sifuni Mchome amewataka watumishi
wa ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali kuzingatia ushirikishwaji katika
ngazi zote sambamba na kufanya kazi kwa uwazi, huku wakifuata miiko ya
kazi yao.


Prof.
mchome ameyabainisha hayo jijini Dodoma wakati akifungua baraza la
wafanyakazi wa ofisi ya wakili mkuu wa Serikali ambapo amesema kutokana
na unyeti wa ofisi hiyo inahitajika kila mtumishi kufanya kazi wa weredi
huku wakilenga kutafuta matokeo.


“mfuate
maadili ya kazi yenu maadili yanakusaidia katika kutekeleza majukumu
yako kikamilifu, sekta yenu ni muhimu sheria ikisimama na hata nchi
itatulia” amesema Prof. Mchome.


Amesema
mabaraza ya wafanyakazi ni muhimu sana katika maeneo ya kazi kwa sababu
huko ndiko ushirikishwaji utafanyika ni muhimu kila taasisi iwe na
mabaraza hayo ambayo yapo kwa mujibu wa sheria.


“Serikali
itahakikisha taasisi zake zote zinatekeleza takwa hili la sheria la
kuwa na mabaraza ya wafanyakazi huku ndiko kutafanyika ushirikishwaji
katika mambo mbalimbali kwa watumishi katika ngazi zote” amesema.


Amesema
katika majukumu yao wafanye kazi wakilenga kupata matokeo chanya katika
kutafuta ushindi katika kesi mbalimbali ambazo wanazisimamia katika
ofisi zao zilizopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.


Amewataka
kujenga utaratibu wa kufanya tathmini za mara kwa mara katika kazi
wanazozifanya ili kuona namna ya kuboresha kazi zao kwani bila tathmini
hawawezi kupata kile walichokusudia katika sekta ya sheria hapa nchini.


Ameongeza
kuwa “mkasikilize kero za wananchi tunakofanya ziara huko mikoani
malalamiko ni mengi, naamini huko mnaofisi zenu mkashughulikie hayo
malalamiko ni mengi sana” amesema.


Aidha
amewataka wataalamu hao kwendana na kasi ya sasa na sio kufanyakazi kwa
mazoea kwani kwa sasa nchi imeingia katika uchumi wa kati hivyo nao
wabadilishe namna ya ufanyaji kazi ili kuendana na kasi ya uchumi wa
kati ili kama nchi kupata mafanikio zaidi.


Awali
Wakili Mkuu wa Serikali ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo bw.
Gabriel Malata amesema kikao hicho ni cha pili kwa mwaka wa fedha 2020
-2021, ambao wanakutana kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali
yanayohusu ofisi hiyo.


Pia
amebainisha kuwa ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali ilianzishwa Feb, 12,
2018 na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dkt John Magufuli na
kupewa jukumu la kuendesha, kuratibu, na kusimamia mashauri mbalimbali
yanayohusu Serikali na taasisi zake.


Amesema
katika kipindi cha mwezi julai 2020, hadi Feb, 2021 ofisi hiyo
imeshughulikia jumla ya mashauri 3715, kati ya hayo mashauri ya madai ni
3625 na 90 ni ya usuluhishi, jumla ya mashauri 451 kati ya 3715
yaliendeshwa na kumalizika.


Kati
ya mashauri hayo 422 ni ya madai ambayo yanajumuisha mashauri 418 ya
madai ya ndani ya nchi yakiwamo 13 ya uchaguzi na mashauri manne (4)ya
madai ya nje ya nchi, na kukamilika kwa mashauri hayo kumepelekea kuokoa
zaidi ya shilingi bilioni 643.7, ambazo zingelipwa na serikali kama
ingeshindwa.


Aidha
amesema ofisi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ya
kukosa muundo wa uendeshaji wa ofisi hiyo ambapo kwa sasa wanatumia
muundo wa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.