Prof. ndalichako afungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha skauti tanzania


Skauti
Mkuu wa Tanzania, Mwantumu Mahiza, akizungumza katika Mkutano Mkuu wa
Mwaka wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
Desemba 4, 2019.


Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania.

Wajumbe wa mkutano mkuu wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani).

Wajumbe wa Bodi.

Mkutano ukiendelea.
 

Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza
wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika
jijini Dar es Salaam leo Desemba 4, 2019.


Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, akipongezwa na
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, baada ya kutoa hotuba
yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania.


Kamishna
Mkuu wa Chama cha Skauti, Grace Kado, akimkabidhi zawadi ya picha ya
mwazilishi wa Skauti duniani, Baden-Powell, Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Desemba 4, 2019.


Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hssan Mwinyi, ambaye pia ni Mdhamini wa
Chama cha Skauti Tanzania, akipokea zawadi ya picha ya Baden-Powell
ambaye ni mwanzilishi wa skauti duniani kutoka kwa Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako.


Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hssan Mwinyi, ambaye pia ni Mdhamini wa
Chama cha Skauti Tanzania, akipokea zawadi ya picha ya mwanzilishi wa
skauti duniani, Baden-Powell, kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako.


Meza Kuu.

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi.

Picha ya pamoja.


Picha ya pamoja.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, Rais Mstaafu
wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ambaye pia ni Mdhamini wa Chama cha
Skauti Tanzania, baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Skauti
Tanzania.

Skauti kutoka Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere wakiimba ngojera katika mkutano huo.

Skauti wakicheza na kuimba nyimbo za kitamaduni.




Na Asha Mwakyonde


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako,
amekitaka Chama cha Skauti Tanzania kuanzisha miradi ya kilimo cha mboga
mboga kwa lengo la kuinua kipato na kuwawezesha vijana wa chama hicho
kuwa na uelewa wa kufanya kazi.



Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Desemba 4, 2019, wakati akifungua
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho amesema uanzishwaji wa mradi huo
utawajengea vijana hao utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii.



Prof. Ndalichako amesema uongozi wa chama hicho ukiwa na ubunifu na nia
thabiti ya kukabiliana na changamoto hakika vijana watajifunza mambo na
namna ya kujenga taifa lao kwa ari moja.



“Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuwafundisha vijana hao
namna ya kuwapatia elimu ambayo inawafanya watambue mambo ambayo hayafai
katika taifa hili likiwamo suala la rushwa,” amesema Prof. Ndalichako.



Aidha amewataka wazazi na walezi kuwaruhusu watoto wao kujiunga na
chama hicho ambayo kimekuwa kikiwafundisha vijana maadili mema na
kupinga rushwa.



Awali Mkuu wa Skauti Tanzania, Mwantumi Mahiza, amesema kuwa katika ili
kutatua tatizo la rushwa nchini hasa kwa kuwaandaa vijana tayari
wameingia makubaliano na Taasisi ya kuthibiti na kupamba na Rushwa
Tanzania (TAKUKURU), kutoa elimu kupitia skauti katika shule za msingi
na sekondari nchini.



” Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2019 kutoka Wizara ya elimu tunazo
jumla ya shule za msingi za serikali na binafisi ni 17,804 zenye
wanafunzi 10,617,373,amesema Mwantumu.



Ameongeza kuwa wanazo shule za sekondari za serikali na binafisi kidato
cha kwanza hadi cha nne zipatazo 5,716 zenye jumla ya wanafunzi 2,
595,902 na kwamba wanatarajia kuwafikishia elimu hiyo juu ya madhara ya
rushwa na namna ya kupambana nayo wanafunzi hao 13,213,275.



Amesema kuwa lengo la chama hicho ni kuisaidia jamii ya Watanzania kuwa
na vijana wazalendo wenye uchungu na nchi yao na kwamba kupitia skauti
watajenga Taifa lenye vijana mahiri wenye weledi wakutosha na waadilifu
kwa nchi yao.