Profesa mbarawa nitazivunja bodi za maji zitakazoshindwa kukusanya mapato ya maji

SALVATORY NTANDU,SHINYANGA
Waziri
wa Maji, Profesa Makama Mbarawa asema ataifuta bodi mpya ya Maji ya
Malmlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) 
endapo itashindwa kukusanya mapato kutoa shilingi milioni 691 za sasa
hadi kufikia milioni 700.

Uamuzi
huo ameutoa jana mjini Shinyanga katika hafla ya kuipitisha bodi hiyo
mpya ambayo imeanza kazi rasmi ya usimamizi na uendeshaji wa shughuli za
Maji katika Manispaa ya shinyanga kwa kipindi cha miaka 3.

“Kama
hamtafikia makusanyo ya mapato ya shilingi milioni 700 ni lazima
niivunje bodi hii, muda wa kubembelezana umekwisha bondi nyingi zimekuwa
zikifanya kazi kwa mazoea kwa kupeana posho na safari amabazo hazina
tija na kushindwa kuzisimamia mamlaka za maji”alisema Profesa Mbarawa.

Kwa
mwaka mamlaka hii inakusanya shilingi zaidi ya shilingi bilioni 5.9 
lakini makusanyo ya mamlaka hii yako chini ikilinganishwa na Idadi ya
watumiaji wa maji ambao ni wengi jambo ambalo linaonesha kuwa katika
Mamlaka hii kuna  uzembe katika usanyaji wa mapato na kuisababishia
serikali kukosa mapato.

“Mwezi
oktoba mwaka jana mmekusanya shilingi milioni 667, septemba 679, 
Agosti 691 fedha hizi hazitoshi ikilinganishwa na maji mnayozalisha 
ambayo ni lita milioni  438 lakini maji  lita milioni 365 ambapo maji
ambayo yanaonekanakupotea njiani ni lita milioni 75  kwa upotevu  lazima
bodi hii mpya ianze kuifanyia kazi suala hili” alisema Profesa Mbarawa.

Waziri
mbarawa aliongeza kuwa ni lazima mamlaka zote nchini kuhakikisha
zinaongeza makusanyo kwa kuanzisha miradi ya mipya ya maji ikiwa ni
pamoja na kuongeza matandao wa maji ili kuhakikisha watanzania wote
wanapata huduma za maji karibu na maeneo yao.

Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA Flaviana Kifizi alisema kuwa
watahakikisha wanadhibiti upotevu wa maji kwa kushirikiana na Bodi mpya
chini ya Mwenyekiti Mwamvua Jirumbi kwa kutekeleza maagizo yote ambayo
yametolewa na serikali ili kuboresha utendaji kazi utakaosaidia
kuongezeka kwa mapato.

Amefafanua
kuwa SHUWASA inatekeleza miradi ya maji katika wilaya za Kahama kwenda
ngogwa hadi kitwana,na Katika wilaya ya Shinyanga ni kutoka Negezi hadi
Mwawaza kwa kuwatumia wataalamu wa ndani kupitia Force account ambapo
miradi hii imefikia katika  hatua mbalimbali na mafundi wapo katika
maeneo ya Miradi.

Nae
mwenyekiti aliyemaliza muda wake Deogratius Sulla alisema taasisi za
umma zinasuasua kulipa madeni ya Ankara za maji za kila mwezi na
kusababisha deni kuendelea kuongezeka hadi kufikia shilingi mlioni 949.

“Mpaka
mwezi Disemba mwaka jana JWTZ ilikuwa inadaiwa shilingi milioni
520,244,957,Magereza shilingi milioni 256,520,120,Polisi shilingi
172,346,465”alisema Sulla.

Bodi ambayo imemaliza muda wake ilizinduliwa rasmi Novemba 14 mwaka 2016.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *