Rais magufuli aagiza askari wa kike wp 4160 beatrice kayuni mlanzi apandishwe cheo


Rais
Magufuli ameagiza WP 4160 Beatrice Kayuni Mlanzi, kupandishwa cheo
kutoka Koplo na kuwa Sajenti baada ya kuonesha utimilifu katika kazi.


Agizo hilo amelitoa jana Septemba 10, 2019, baada ya kupita katika kituo cha Polisi Selander Bridge.

Rais
Magufuli alipita kituoni hapo akiwa njiani kurejea Ikulu, akitokea
Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokwenda
kumjulia hali Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi.

Rais
alimjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu
Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi hiyo ya
MOI mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa Kichwa.
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *