Rais magufuli amkabidhi naibu mkurugenzi wa takukuru ripoti ya miradi 107 yenye dosari

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi
Naibu Kamishna wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo ripoti
aliyokabidhiwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa wakati wa hotubia
yake kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na
Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
zilizofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi Oktoba 14,
2019

                                                                            

***
Rais  
Magufuli amemkabidhi naibu mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali
John Mbungo ripoti ya miradi 107 iliyobainika kuwa na dosari.


Miradi
hiyo ilibainika kuwa na kasoro ilipotembelewa kwa ajili ya kuzinduliwa
na kukaguliwa katika mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofikia kilele chake
leo Jumatatu Oktoba 14, 2019.
Rais
Magufuli amekabidhi ripoti hiyo leo katika maadhimisho ya kilele hicho
na kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere
yaliyofanyika mkoani Lindi.
Awali,
kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Mzee Mkongea Ally alimkabidhi Rais
Magufuli ripoti ya miradi ya Sh90.28 bilioni iliyokutwa na dosari.

“Sogea
hapa mbele nikukabidhi ripoti hii, zege halilali. Naikabidhi hii ripoti
ukafanye ukaguzi kila ukurasa, kila nukta na ukachambue wale wote
wanaohusika wapelekwe mahakamani. Usisite wapeleke mahakamani,” amesema
Rais Magufuli wakati akimkabidhi Brigedia  Jenerali Mbungo ripoti hiyo.