Rais magufuli ampa maagizo mazito cag mpya…..” usijifanye muhimili…sikutishi…..”

Rais Dkt. John Pombe Magufuli
amemuapisha Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere,
leo Novemba 4 ,2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumpa maagizo katika
kazi yake mpya.
Moja ya maagizo aliyompa ni kuhakikisha
anasuka upya uongozi ndani ya taasisi hiyo ili kuhakikisha kuwa inafanya
kazi kulingana na sheria na maagizo ya mihimili inayoongoza nchi. 
Maagizo mengine aliyopewa ni, “CAG nenda
kafanye kazi huko, usije ukajifanya na wewe ni muhimili mwingine,
mihimili ni mitatu na umeshaiona hapa. Nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa
Serikali, kafanye kazi zako vizuri bila ya kuonea watu. 

“Unapopewa kazi na mihimili mingine kama
Bunge au Mahakama kaitekeleze usibishane nao wewe ni mtumishi.
Kasimamie hiyo ofisi kuna baadhi ya watendaji wako wanapokwenda kukagua
kwenye balozi wanaomba fedha, sasa nenda kawachambue.” Amesema Rais
Magufuli.
Aidha, amesema Rais ana mamlaka ya
kumtoa CAG kulingana na Katiba na Sheria akieleza kuwa upo uwezekano wa
mtumishi wa nafasi hiyo kutolewa muda wowote hata chini ya miaka mitano.

“Nenda ukachape kazi, katika maisha ya
duniani huwezi kupewa mamlaka ya kuteua halafu usiwe na mamlaka ya
kutengua, ukishindwa hivyo huwezi kuwa Rais. Mwenzako aliyekuwepo
amemaliza muda wake leo, kwa hiyo kesho uende ofisini ukaanze kazi,
kayatoe mauchafu yote utakayoyakuta mengine waulize Wizara ya Fedha
wanayafahamu,” amesema Rais.
“Unaweza kumaliza miaka yako mitano au
ukaishia mmoja. katika maisha ya duniani huwezi ukapewa mamlaka ya
kuteua halafu usiwe na mamlaka ya kutengua, sikutishi lakini wewe nenda
kafanye kazi zako” 
Kuhusu suala la rushwa, Rais Magufuli
amesema, “lakini pia kasimamie hiyo ofisi kuna baadhi ya watendaji wako
wanapotumwa kwenda kukagua kwenye balozi wanalipwa pesa hapa na wakifika
huko nako wanaomba pesa. 
Ofisi
ya CAG sio clean (safi) kama mnavyofikiria, sasa nenda kachambue
ukapange positions (nafasi) za watu wako, ili mauchafu (uchafu) haya
ukayasafishe.
“Una heshima umetolewa kwenye Ukamishna
wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) hukusema neno ukaenda kufanya kazi
huko, wapo wengine ukiwateua utadhani nafasi zao unampa UDC (Ukuu wa
Wilaya) ukimtoa anaanza kulalamika,” amesema Rais Magufuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *