Rais magufuli ashauri wanaotuhumiwa kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha wakiri makosa yao na waachiwe huru

Rais
Magufuli ameshauri mahabusu wa makosa mbalimbali hasa ya uhujumu uchumi
na utakatishaji fedha ambao wapo tayari kuomba msamaha na kurudisha
fedha walizotakatisha, wasikilizwe ndani ya siku saba kuanzia kesho
Jumatatu Septemba 23 hadi Jumamosi ya Septemba 28, 2019.

Magufuli
ameyasema hayo leo Jumapili Septemba 22, 2019 Ikulu jijini Dar es
Salaam mara baada ya kumaliza kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua
Ijumaa iliyopita ya Septemba 20, 2019.
“Mimi
naumia kuona watu wapo mahabusu au watu wamefungwa. Ni bahati mbaya kwa
sababu sheria zipo. Lakini mtu anapowekwa mahabusu inaumiza sana,”
amesema Magufuli.
Kutokana
na hilo, Magufuli amemwagiza Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania
(DPP), Biswalo Mganga na wote wanaohusika na sheria kuwasikiliza
mahabusu wenye kesi za uhujumu uchumi ambazo hazitawafanya kutoka mapema
kwa mujibu wa sheria na kama itaruhusu watoke.
Amewataka
kutengeneza mazingira watu hao warudishe fedha zote walizochukua kwa
sababu wanateseka kukaa mahabusu miaka hadi mitatu na wengine wamekonda.
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *