Rais magufuli atamani msanii harmonize akagombee ubunge tandahimba

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika ziara yake mkoani Lindi, Wilaya ya Ruangwa jana Oktoba 15, 2019 alisema anatamani msanii Rajabu Abduli maarufu kama Harmonize kugombea Ubunge Jimbo la Tandahimba.

Akitoa shukrani na pongezi kwa watu waliotoa burudani katika mkutano huo, Rais Magufuli alisema “La kumalizia nawapongeza sana waimbaji hawa wakina baba, lakini nampongeza sana Harmonize sijui anatoka jimbo gani?

“Anatoka jimbo gani huyu? Tandahimba? Mbunge wa kule ni nani?. Aaa ningetamani kweli Harmonize akagombee kule akawe mbunge wa Tandahimba” alisema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *