Rais magufuli atangaza kuhamia rasmi dodoma


Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo
amehamia rasmi Jijini Dodoma na kwenda kujiandikisha kwenye daftari la
orodha ya wapigakura katika kituo cha Sokoine kitongoji cha Sokoine
wilayani Chamwino.

Loading…

UWT yasisitiza madaraka 50 kwa 50
Akizungumza na wananchi waliokuwepo kwenye kituo cha kujiandikishia,
Rais Magufuli amesema ameshahamia rasmi makao makuu ya nchi na kuwaahidi
wananchi wa Chamwino kuwa tatizo la maji walilonalo litafanyiwa kazi
haraka.

” Nimehamia rasmi Dodoma, nimejiandikisha katika eneo langu na nitapiga
kura hapa hapa tarehe 24 kuwachagua viongozi wangu wa mtaa” amesema Rais
Magufuli.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2016 Serikali ya awamu ya tano ilihamia rasmi
jijini Dodoma na Aprili 2019 Rais Magufuli alizindua mji mpya wa
Serikali, ambao ndiyo makao makuu ya wizara zote.