Rais magufuli atuma salamu za rambirambi kifo cha rais mstaafu wa kenya arap moi

Rais 
Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa niaba ya Watanzania kwa Rais
wa Kenya, Uhuru Kenyatta kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa pili wa
nchi hiyo, Daniel Arap Moi (95).


Moi
amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Februari 4, 2020 katika
Hospitali ya Nairobi, Kenya alikokuwa anapatiwa matibabu.

Rais
Magufuli ametumia akaunti yake ya Twitter kutuma salamu hizo akisema,
“kwa niaba ya Serikali na Watanzania nakupa pole Mhe. Rais Uhuru
Kenyatta na Wakenya wote kwa kuondokewa na Rais mstaafu Daniel Toroitich
arap Moi.”

“Watanzania
tutamkumbuka kwa uongozi wake mahiri, jitihada za kuimarisha uhusiano
wetu na Kenya na kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki,” ameandika Rais
Magufuli