Rais magufuli : baadhi ya viongozi wa dini wameanza kuyumba..wamemsahau mungu kwenye corona


Rais
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema baadhi ya viongozi wa dini
wameanza kuyumba na kumsahau Mungu katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa
Corona.


 Rais
Mafuguli ameyasema leo Jumapili Mei 3,2020 akiwa Chato Mkoani Geita
wakati wa hafla fupi ya kumuapisha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa
Katiba na Sheria.

Malunde
1 blog imefuatilia hotuba ya Rais Magufuli iliyokuwa inarushwa Live
katika vyombo vya na imefanikiwa kupata nukuu zifuatazo

⇒⇒⇒”Wapo
hadi baadhi ya viongozi wa dini wamemsahau Mungu ambaye kila siku
wamekuwa wakituhubiria, wanashika vitabu wanafahamu yupo Mungu” – Rais
Magufuli.

⇒⇒⇒Leo
kuna baadhi ya viongozi wa dini wameanza kuyumba na kumsahau Mungu
ambaye waliapa ndiyo kiapo chao Biblia au Quraan,wameanza kuisahau na
kuiweka pembeni na kuuweka ubinadamu mbele.. Acheni kuomba
tunajiokoa,acheni sijui nini nini..

⇒⇒⇒Ni
mambo ya ajabu lakini ndiyo hivyo katika kipindi hiki cha mpito
tutayasikia mengi na huu ndiyo wakati wa kuwapima imani viongozi
tulionao.. Hata viongozi wa dini ..ukizuia waumini wako wasiende
kanisani,ukazuia waumini wako wasiende msikitini na unaweza ukakuta hata
huo msikiti wala hukuujenga wewe,umejengwa na hao waumini..hilo nalo ni
suala la ajabu la kujiuliza, si uwafungulie hao waumini wenye nia
waende mle wakamuombe Mungu hata kama wewe hutaenda kuhubiri pale?

⇒⇒⇒Ndiyo
hapa tutayaona, na hizi ni changamoto..Tuendelee kumuomba Mungu na
Mungu atatusaidia katika kutupitisha kwenye changamoto hizi wala hali
siyo mbaya kama inavyotishwa sisi tupo vizuri na biashara zinaendelea na
ndiyo maana tuna uwezo wa kulipa hata mishahara” – JPM

⇒⇒⇒Tufunge
kila kitu utawalipa mishahara? hata wanaozungumza hao funga huku
wanaendesha magari yameandika STK,mafuta yanawekwa mule na serikali
lakini anasema fungeni,amesahau alichokalia ndiyo kinachomlisha..

⇒⇒⇒Watanzania simameni Imara,huu ugonjwa utaisha,utapita tunapata changamoto lakini tunazitatua.