Rais magufuli kuwa mgeni rasmi mkutano wa wakuu wa polisi mashariki mwa afrika

Na Woinde Shizza,Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21  wa  Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika Septemba 19 mwaka huu.


Katika Mkutano huo ulioanza septemba 15 kwa wakuu wa vitengo mbalimbali vya polisi kukutana Arusha, Msemaji wa Jeshi la Polisi
(SACP)David Misime amesema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika.

Alisema
kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo kutatanguliwa na vikao mbalimbali
vya wakuu wa vitengo vya Interpol na Septemba 16/17 kutakuwa na mkutano
wa wakurugenzi wa upelelezi (DCI)kutoka nchini 14 pia kutakuwa na kikao
cha kamati ndogo cha wataalam wa mafunzo  , wataalamu wa sheria na kikao
cha wa kujadili unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kikao cha Kuzuia na
Kupambana na ugaidi

Alisema
kauli mbiu kuimarisha ushirikiano na ubunifu katika kupambana na
uhalifu unaovuka mipaka ikiwemo makosa ya kimtandao,ugaidi”

Alisema
maandalizi ya mkutano huo yapo vizuri chini ya msimamizi wa Mkoa wa
Arusha,Mrisho Gambo na jana wamekaa na wataalamu wa Interpol kutoka
Kenya ambao wamefanya kikao

Pia
watawapeleka wageni wa mkutano huo chuo cha Polisi Moshi kwaajili ya
kuona madarasa mapya na majengo ya hosteli lengo ni kuongeza wanafunzi
wengi zaidi kutoka nchi mbalimbali

Pia
watawapeleka Gereza la Karanga lililopo Moshi Mkoani Kilimanjaro
kwaajili ya kujionea utengenezaji wa viatu vinavyotumiwa na majeshi
mbalimbali huku wengine wakuu wa Majeshi ya Polisi  wakienda kutembelewa
Hifadhi ya Ngorongoro kujionea Utalii uliopo Nchini
Alisema
Septemba 20 kutakuwa na kikao cha mawaziri wa mambo ya ndani kutoka
nchi hizo na alitoa rai kwa watanzania kuimarisha amani na utulivu 

Mada
zitakazojadiliwa ni kuongeza ushirikiano kwa uhalifu unaovuka mipaka
ikiwemo mikakati ya kutoa mafunzo kwa askari wao kwani hivi sasa Sayansi
na teknolojia imekuwa pamoja na kuangalia maazimio waliyoyatekeleza
katika kikao kilichofanyika mwaka jana nchini Sudani huku Mkuu wa Jeshi
la Polisi Nchini (IGP)Sirro akikabidhiwa rasmi uenuenyekiti mkutanor huo