Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
RAIS
Dkt. John Magufuli amewataka Viongozi wa Bara la Afrika kubadili fikra
na mtazamo wa kutegemea misaada na utegemezi wa kiuchumi kutoka nchi
tajiri na badala yake kutumia diplomasia ya uchumi kuwa msingi wa
ushirikiano katika kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi wake.

Akizungumza
katika ufunguzi wa Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi
za NORDIC na Bara la Afrika ulioufunguliwa leo Ijumaa (Novemba 8, 2019)
Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema uhuru wa kisiasa uliozipata
Nchi za Bara la Afrika hautakuwa maana iwapo Nchi zake zitaendelea klwa
wategemezi wa misaada kutoka Nchi tajiri.

Rais
Magufuli alisema kuwa Bara la Afrika lina mambo mengi mazuri
yanayopaswa kuwekewa kipaumbele katika kujikwamua kiuchumi kupitia
ushirikiano wake na Nchi za NORDIC ikiwemo fursa za biashara na
uwekezaji, hivyo kuliweka katika ajenda muhimu inayopaswa kuwekeza
msisitizo.

‘Ushirkiano
wetu na Nchi za NORDIC kwa miaka mingi umekuwa ni utegemezi wa
kiuchumi, Viongozi wa Afrika tunapaswa kutambua kuwa mustakabali wa
mataifa yetu upo mikononi mwetu, ni lazima tuondokane na aina hii ya
ushirikiano’’ alisema Rais Magufuli.

Aidha
Rais Magufuli alisema Bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa raslimali
na vivutio mbalimbali vya biashara na uwekezaji ukilinganisha na Nchi za
NORDIC, lakini hata hivyo Mataifa hayo ya NORDIC yamekuwa yakipiga
hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi ikilinganisha na Nchi za Bara la
Afrika.

Akitoa
mfano Rais Magufuli alisema katika Nchi tano za NORDIC zenye ukubwa wa
kilometa za mraba Milioni 3.5 na mwaka 2018 zilikuwa na Pato la Taifa
la Dola Trilioni 1.7 kwa mwaka huku idadi ya wananchi wake ikiwa ni
Milioni 27 wakati Bara la Afrika lenye watu Bilioni 1.2 mwaka 2018
lilikuwa na Pato la taifa lenye thamani ya Dola trilioni 2.334, na
kuongeza kuwa Nchi za Bara la Afrika lipo jambo linalopaswa kujifunza.

Rais Magufuli alisema ni wajibu wa Viongozi wa Bara la Afrika kuweka
nguvu ya pamoja katika kusimamia rasilimali na maliasili ilizonazo kwa
ajili ya kuleta ustawi wa maendeleo katika sekta mbalimbali za kiuchumi
ikiwemo kilimo, madini, misitu, mafuta, gesi, nishati na mifugo

‘Asilimia
30 ya ardhi bora ya kilimo duniani ipo Afrika, na kwa mujibu wa takwimu
zilizopo Kati ya Nchi 10 bora zinazoongoza kwa kasi ya ukuaji uchumi
duniani, Nchi 5 zinatoka Bara la Afrika, hii ni fursa ambayo haina budi
kuitumia Afrika katika kuleta maendeleo kwa ustawi wa wananchi’’ alisema
Rais Magufuli.

Akifafanua
zaidi Rais Magufuli alisema Tanzania kwa upande wake imepiga hatua
kubwa za maendeleo katika Nchi za Bara la Afrika kwa kuwa imeimarisha
sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wake ikiwemo ujenzi
wa miundombinu ya usafiri na kuweka mazingira bora ya uwekezaji.

aliwataka Viongozi wa NORDIC kutumia fursa zilizopo katika Bara la
Afrika kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa viwanda vya malighafi, kwa kuwa
bidhaa nyingi za Afrika zimekuwa zikisafirishwa kwenda kuuzwa nje ya
Nchi, hivyo wawekezaji hawana budi kuitumia fursa hiyo kwa ajili ya
kuleta maendeleo ya Bara la Afrika.

Kwa
upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
wa Tanzania, Prof. Palamagamba Kabudi alisema kwa miaka mingi sasa Nchi
za NORDIC zimekuwa rafiki wa kweli kwa Nchi za Bara Afrika ikiwemo
Tanzania ambapo tangu uhuru wa Tanzania Nchi hizo zimekuwa zikisaidia
ujenzi wa miradi mbali ya maendeleo nchini.

mujibu wa Prof. Kabudi alisema katika Mkutano huo, Mawaziri wa Nchi za
NORDIC na wale wa Bara la Afrika watapata fursa ya kujadiliana masuala
mbalimbali ikiwemo diplomasia ya uchumi na masuala ya ulinzi na usalama
na kuweka mkakati wa pamoja utakaowezesha nchi hizo kufikia malengo
waliyojiwekea.

‘Suala
la Mpango wa Maendeleo Endelevu wa mwaka 2030 pia ni moja ya maeneo
yatakayojadiliwa na Mawaziri wa Nchi hizi, tutaliangalia kwa undani
zaidi suala la mabadiliko ya tabia nchi katika namna bora ya kukabiliana
na changamoto zake katika Mataifa yetu ya Bara la Afrika’’ alisema
Prof. Kabudi.

Naye
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Ine Eriksen Soreide alisema Nchi za
NORDIC zitaendelea kushirkiana na Mataifa ya Bara la Afrika katika
kuleta maendeleo ya wananchi pamoja na mipango ya pamoja ya kukabiliana
na matishio mbalimbali ya binadamu ikiwemo ugaidi na magonjwa ya
milipuko.

Nchi
za NORDIC zitaundwa na Nchi tano za Sweden, Norway, Finland, Iceland na
Denmark pamoja ikiwa na ushirikiano wa Nchi 29 za Bara la Afrika.