Rais wa zamani wa sudan, omar al-bashir ahukumiwa miaka miwili jela kwa rushwa

Mahakama
ya nchini Sudan imemkuta Rais wa zamani Omar al-Bashir na hatia ya
makosa ya utakatishaji fedha na rushwa na kumhukumu kifungo cha miaka
miwili gerezani. 


Hiyo
ni hukumu ya kwanza katika msururu wa kesi zinazomkabili al-Bashir,
ambaye pia anasakwa na mahakama ya Kimataifa ya Jinai – ICC kuhusiana na
mashitaka ya uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki yanayohusiana na
mgogoro wa Darfur katika miaka ya 2000. 

Hukumu
ya leo inakuja ikiwa ni mwaka mmoja baada ya waaandamanaji nchini Sudan
kuanzisha vuguvugu la mapinduzi dhidi ya serikali ya kimabavu ya
al-Bashir. 

Wakati
wa miongo yake mitatu madarakani, Sudan iliwekwa kwenye orodha ya
Marekani kwa kufadhili ugaidi, na uchumi wa nchi hiyo ukasambaratishwa
na miaka mingi ya usimamizi mbaya na vikwazo vya Marekani.