Rc arusha apongeza uwekezaji wa tanzania na canada kwenye elimu ya ualimu

Na Ahmed Mahmoud,Arusha.
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mrisho Gambo ameipongeza serikali ya Canada kwa kushirikiana na
Serikali ya Tanzania katika kuboresha elimu ya ualimu nchini kwa kujenga
miundombinu ya majengo,TEHAMA na vifaa vya kufundishia pamoja na mafunzo kwa
walimu kupitia mradi wa (TESP).
Akisoma
risala ya Mkuu wa Mkoa iliyosomwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard
Kwitega amepongeza mafanikio ya mradi huo wa elimu  unaolenga kukuza ubora wa elimu nchini kwa
kuwaandaa walimu bora wataoleta matokeo makubwa kwenye sekta ya elimu nchini.
“Napongeza
Uwekezaji wa Tanzania na Canada katika elimu ya ualimu ambayo  kuanzia kwenye miundombinu hadi mafunzo kwa ualimu
kwani Elimu ni jiko la kupika wataalamu watakaotufikisha kweye ” Alisema
Kwitega
Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Dr.Ave Maria Semakafu  amesema kuwa Mradi huo  wamekutana jijini Arusha kufanya tathmini ya
utekelezaji wa mradi  wa TESP  kwasababu huu mradi umejikita katika
kuboresha taaluma zaidi,mradi wa kuboresha miundombinu uko katika hatua za
mwisho kukamisha.
Pia kuna
fedha zinatolewa kwa ajili ya uendeshaji wa vyuo kitaaluma ,kuna fedha
zinatolewa kwa ajilli ya wanafunzi.
Kamishna wa
Elimu kutoka Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Dkt.Lyabwene Mtahambwa amesema
kuwa Mafunzo ya ualimu ni nguzo muhimu katika kuboresha elimu nchini
,tunawaandaa walimu kwa ubora watakaoleta matokeo mazuri .
“Tunawapa mafunzo
walimu wawe na upendo kwa wanafunzi na kufanya kazi kwa kujitoa bila kusukumwa
ili kufikia mafanikio ya kitaaluma” Alisema Kamishna