Rc chalamila sasa kuwachapa viboko wale hawajaoa au kuolewa

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amesema kwa sasa atakuja na
mpango wa kuwachalaza bakora wanawake na wanaume mkoani kwake, ambao
hawajaoa au kuolewa na kueleza akishamaliza kuwachapa, atawaagiza waende
wakatafute wapenzi wao wa kufunga nao ndoa.
Chalamila ametoa kauli hiyo mkoani Mbeya, ambapo amesema njia ya kutumia
bakora ni miongoni mwa njia ambazo zinasaidia sana kwenye kuhamasisha
jambo.
“Siku hizi tunatumia bakora katika kila jambo, tukikukuta umekaa
nyumbani na huolewi ni bakora tu nenda katafute mume na ukiwa umekaa
nyumbani huoi ni bakora tu nenda katafute mke, kuna umri ambao unatosha
lazima uchangamshwe” amesema Chalamila.
Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa huo, alitawala kwenye vyombo mbalimbali vya
habari baada ya kuonekana anawachapa bakora baadhi ya wanafunzi wa Shule
ya Sekondari Kiwanja, iliyopo Chunya mkoani Mbeya, baada ya kuteketeza
kwa moto mabweni yao.