Rc makonda awapa miezi mitatu jkt kukamilisha ujenzi hospital ya wilaya ya ubungo

Siku chache baada ya
Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5
kwaajili ya Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Ubungo, Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelea na kukagua eneo
itakapojengwa hospital hiyo na kuwaekekeza JKT kuhakikisha wanafanya
kazi usiku na Mchana na kukabidhi jengo ndani ya Miezi mitatu kuanzia
leo ili wananchi wa wilaya hiyo wapate huduma Bora za Afya.
RC Makonda amesema
Hospital hiyo inajengwa eneo la Kimara Baruti kwenye eneo lenye ukubwa
wa Hekari 5.5 ambapo amemshukuru Rais Magufuli Kwa moyo Wa Upendo
anaoendelea kuonyesha kwa Wakazi wa Dar es salaam na Wilaya ya Ubungo.
 
Aidha RC Makonda
amesema kuwa maandalizi yote ya ujenzi yamekamikika na kazi ujenzi
itaanza rasmi kesho huku akibainisha kuwa kukamikika kwa Hospital hiyo
kutasaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza changamoto za Afya Wilayani humo.

Itakumbukwa Juzi
October 26 wakati wa hafla ya Kupokea ndege ya 8 Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe. Paul Makonda alitumia hafla hiyo kuwasilisha kilio cha
wakazi wa Ubungo juu ya kukosekana kwa hospital ya wilaya ya Ubungo
ambapo Rais Magufuli alipokea kwa mikono miwili ombi hilo na Kumuelekeza
Waziri wa TAMISEMI kutoa fedha hizo na hatimae leo utekelezaji wa
ujenzi unaanz