Rc mongella azindua maadhimisho ya maulid kitaifa jijini mwanza

Mkuu wa Mkoa
Mwanza, John Mongella (katikati) amezindua rasmi wiki ya maadhimisho ya sikukuu ya Maulid
inayofanyika kitaifa jijini Mwanza. 
Uzinduzi huo
ulifanyika Novemba 04, 2019 katika uwanja wa Furahisha ambapo Sikukuu ya
Maulidi inatarajiwa kufanyika Novemba 09, 2019.


Sikukuu
ya Maulid mara ya mwisho ilifanyika mkoani Mwanza zaidi ya miaka 20
iliyopita hivyo kufanyika mwaka huu 2019 (1441) ni neema kubwa huku
jambo jema zaidi likiwa ni ushirikiano baina ya dini zote.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akionesha kanga zenye ujumbe wa Maulid 2019 kama ishara ya uzinduzi wa sikukuu hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Maulid.
Sheikh
Issa Othuman Issa kutoka Baraza la U’lamaa BAKWATA akitoa salamu zake
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua Maulid 2019.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa Maulid kitaifa jijini Mwanza.
Mkuu
wa Mkoa Mwanza (wa pili kushoto) akipata maelezo baada ya kutembelea
banda la Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI
ambalo ni miongoni mwa wadau walioshiriki maonesho ya wiki ya Maulid
2019.
Tazama Video hapa chini