MKUU wa Mkoa wa
Dodoma,Anthony Mtaka ,akizungumza na wahitimu katika Mahafali ya tano
ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony
Mtaka,akisisitiza jambo kwa wahitimu wakati akizungumza nao katika
Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo
jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational
Training Centre,Jemima Nchimbi,akisoma risali wakati wa Mahafali ya tano
ya chuo hicho kilichopo jijini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wakifatilia hotuba
ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati
akizungumza katika Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational
Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka
akikata keki wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational
Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka
akilishwa keki na Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training
Centre,Jemima Nchimbi wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha
Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational
Training Centre,Jemima Nchimbi akiwa katika meza kuu na baadhi ya
viongozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka (hayupo
pichani) wakati wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational
Training Centre kilichopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony
Mtaka,akiwa na Mkuu wa Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima
Nchimbi pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa meza Kuu wakati wa
Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo
jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony
Mtaka,akimsikiliza Kiongozi wa Wazee Bw.Ezekiel Chadwanga wakati wa
Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre kilichopo
jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony
Mtaka,akisimikwa Wazee Bw.Ezekiel Chadwanga kuwa kiongozi wao wakati
wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational Training Centre
kilichopo jijini Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony
Mtaka,akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka katika uongozi wa Chuo cha
Dodoma,Vocational Training Centre mara baada ya kuhudhuria Mahafali ya
tano ya chuo hicho kilichopo jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka
akigawa vyeti kwa wahitimu mbalimbali kulia kwake ni Mkuu wa Chuo cha
Dodoma,Vocational Training Centre,Jemima Nchimbi wakati wa Mahafali ya
tano ya Chuo hicho kilichopo jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………
Na Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa Mkoa wa
Dodoma,Anthony Mtaka amewataka vijana wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha
wanakuwa na ujuzi ili kwendana na kasi ya Mkoa huo kuwa Makao Makuu ya
Nchi.
Akizungumza
leo,Julai 22,2021,katika mahafali ya tano ya Chuo cha Dodoma,Vocational
Training Centre(Dodoma VCT)Mkuu huyo wa Mkoa amewataka vijana wa Mkoa
huo kuwa na ujuzi ili kuzikimbilia fursa mbalimbali ambazo zitapatikana
kutokana na Mkoa huo kuwa Makao Makuu ya Nchi.
“Wito wangu kwa
vijana wa Mkoa wa Dodoma niwatake kuwa na ujuzi katika Makao Makuu ya
Nchi niwatake kila mmoja apate ujuzi tumieni vyuo vya kati wazazi
niwaombe watoto wapate ujuzi kama hajafaulu apate nafasi ya kusoma
ujuzi wowote, Dodoma na Dunia tunayoiendea itakuwa na fursa nyingi
lakini kama huna ujuzi utapishana na fursa
“Mtu anaenda Garage
anakuwa ni msafisha vioo lakini baadae anajifunza umakenika baadae
anajifunza udereva anakuwa dereva,vijana wengi ni bodaboda wewe
(wahitimu) kuwa fundi bodaboda utakuwa umepata ajira lazima vijana
mhakikishe mna ujuzi na kuna kozi zingine ni fupi tu,”amesema Mkuu huyo
wa Mkoa.
“Dodoma ni Makao
Makuu hivyo mnafaida mjiandae miradi inayokuja ikukute una ujuzi hapa
ujenzi ni mkubwa sana kama unakaa nyumbani hakuna kibarua ni wewe
tu,tumia fursa.Tunajenga hapo Msalato likiwanja likubwa kabisa
wakikuuliza una ujuzi wewe upo tu tafuta ujuzi.
“Kama unakaa hapa
usidhani unapoteza muda kuna siku utamkumbuka huyu mama wazazi viombeeni
hivi vyuo vya ujuzi kama kuna mtu anakudanganya fundi amekosa ajira
huyo anakudanganya.Kama unasoma ujuzi shikilia hivyo ninyi hamjapoteza
na wazazi mliopo nyumbani usikae na mototo ambaye hana ujuzi.
“Nakuombea Madame
kazi zote duniani tunaanzia chini kazi moja tu ndio unaanzia juu kwenda
chini kazi hiyo ni kuchimba kaburi na hapa tumeanza.Endelea kusoma
mazingira kozi gani utaziongeza ili washindane na tembelea vyuo vingine
uone ambavyo wanavyo wewe huna na mitaala pamoja na walimu,”amesema
Mkuu huyo wa Mkoa
pia amekitaka Chuo hicho kuongeza ubunifu pamoja na kozi mbalimbali ili
watu wengi waweze kupata ujuzi ambao utasaidia kuondokona na
changamoto ya ajira.
“Madame nakushauru
sana ongeza kozi tujitahidi tuweke matangazo kwamba Chuo kinafundisha
kozi hizi na hizi local radio zungumza uwaokoe watoto wa Dodoma,tukitaka
vijana wa Mkoa huu wawe washindani tuwapeleke kwenye elimu zote ya
darasani,ufundi,elimu dunia aghera.Dunia tunayoiendea tunahitaji maeneo
ya namna hiyo nimeona kozi zako ongeza kozi ili watu wajifunze kuwe na
ujuzi”amesema.
Pia,amewataka
wanafunzi licha ya kujifunza masomo mbalimbali pia wanatakiwa kuwa
wabunifu ili wanapomaliza masomo yao waweze kuajirika kirahisi.
“Mjifunze vyote
ujuzi na ubunifu ukienda mahali kutafuta vibarua unakuwa umekamilika kwa
kila kitu,tunapeleka umeme vijiji vyote vya Tanzania kule vijijini
hakuna mafundi maana yake fundi ni wewe.Tunapeleka umeme na maji katika
vituo vya afya bomba likiharibika au kuziba wewe ndio fundi,”amesema.
Kuhusiana na
changamoto ya eneo la ardhi la chuo hicho,RC Mtaka ameutaka uongozi wa
Chuo kwenda makao makuu ya kata ili kukutana na timu ambayo inazunguka
Mkoa wa Dodoma kumaliza changamoto za migogoro ya ardhi.
“Nikuombe kama
utatumia nafasi vizuri,wanalalamikiana waende makao makuu ya Kata ili
waweze kulitatua.Nakuomba uwezekutumia nafasi hiyo kupata muafaka katika
siku hizo 10 ambazo tumeziongeza kwani tulitenga siku 10 na tuliongeza
siku 10 zingine,”amesema RC Mtaka.
Awali akisoma risala
Mkuu wa Chuo hicho,Jemima Nchimbi amesema wanakabiliwa na changamoto
kukosa eneo la kujenga chuo kutokakana na eneo walilolipata kukabiliwa
na mgogoro.
Amezitaja changamoro
zingine ni vijana kutokupata mikopo kwa kozi za ufundi stadi,uelewa
mdogo wa wazazi kutambua kozi zote ni kwa ajili ya jinsia zote.
Amesema mafanikio
ambayo wameyapata ni pamoja na kufundisha vijana 679 wa kozi
fupi,kufundisha vijana wa kike na wa kiume kwa kozi ndefu zaidi ya 333
ambapo vijana 1002 wameweza kupata mafunzo ambapo asilimia 75
wameajiriwa na asilimia 25 wamejiajiri.
Vilevile,amesema
wamefanikiwa wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa kina mama zaidi ya 197 kwa
kozi za ujasiriamali na baadhi yao wamefungua maduka na kuuza bidhaa
walizojifunza kutengeneza.